Monday, April 1, 2024

PACOME, YAO, AUCHO WATAJWA SULUHU NA MAMELODI


Na John Richard Marwa
Wakati dakika 90 zikitamatika Dimba la Benjamin Mkapa hapo jana kwa Suluhu Yanga SC dhidi ya Mamelodi Sundown, majina ya nyota watatu yametajwa.

Yanga waliingia kwenye mchezo huo wakiikosa huduma ya nyota wao watatu wa kikosi cha kwanza Khalid Aucho, Kwasi Yao na Pacome Zouzua ambao wako nje kwa majeruhi.
Yanga walikuwa na mchezo bora sana katika dakika 90 ambazo zilikuwa za jasho na damu kupepetana na Masandawana lakini wakashindwa kufua dafu.

Majina hayo yanatajwa kutokana na kiwango walivhokionyesha Yanga licha ya kuwakosa nyota hao ambao mashabiki wengi na wadau wa Soka wamekuwa na maoni ikiwa kama wangekuwepo kuongeza kitu Imani ya wengi ushindi ungepatikana.

Kukosekana kwa Yao kulimfanya Kocha Gamondi kuingia na mabeki watatu Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Baka na Dickson Job huku eneo la katikati akiingia Jonas Mkude ambaye alikuwa na mchezo bora sana.

Katika eneo la mwisho nafasi ya Pacome ilimfanya Gamondi kuanza na washambuliaji wawili Clement Mzinze na Kennedy Musonda ambao walikuwa na mchezo bora sana.

Maoni mengi ni kuhusu uwepo wa nyota hao watatu katika mchezo wa marejeano Ijumaa ijayo nchini Afrika Kusini kutaongeza kitu na kuiwezesha Yanga kushinda na kutinga hatua ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL? Ni swali linalosubiri majibu ya dakika 90 za mkondo wa pili

No comments: