Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameshiriki katika kisomo maalum cha Khitma ya kumuombea baba yake Mzazi, Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi iliyoandaliwa na Familia ambayo imefanyika nyumbani kwa marehemu, Mikocheni jijini Dar es Salaam, tarehe 31 Machi 2024.
"Natoa shukrani zangu za dhati kwa waumini wa Dini ya Kiislamu, Viongozi na Wananchi kwa ujumla Tanzania bara na Zanzibar kwa kuendelea kusoma Dua na Khitma ya kumwombea Baba yangu Marehemu Mzee Ali Hassan Mwinyi. Tuendelee kumuombea Dua Marehemu Mzee Mwinyi na wengine waliotangulia mbele ya Haki." Amesema Dkt. Mwinyi, katika salamu zake kwa waliohudhuria kisomo hicho.
No comments:
Post a Comment