Wednesday, June 26, 2024

KONGAMANO LA VYUO VIKUU LAFANYIKA KATIKA WIKI YA MSAADA WA KISHERIA ZANZIBAR


Jaji wa Mahkama Kuu, Zanzibar Mhe. Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim akifungua kongamano la vyuo vikuu la masuala ya msaada wa kisheria, lililofanyika katika Ukumbi wa Aboud Jumbe Tunguu Zanzibar ikiwa ni shamrashamra za maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria, inayofikia kilele chake juni 28.
Mkurugenzi Idara ya Katiba na msaada wa kisheria Zanzibar Hanifa Ramadhan Said akimkaribisha Jaji wa Mahkama Kuu, Zanzibar Mhe. Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim wakati wa kufungua Kongamano la vyuo vikuu la masuala ya msaada wa kisheria, lililofanyika katika Ukumbi wa Aboud Jumbe Tunguu Zanzibar ikiwa ni shamrashamra za madhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria, inayofikia kilele juni 28.
Mkuu wa Seksheni ya usafirisjhaji haramu wa binaadamu Maryam Ali Mohammed akiwasilisha mada ya sharia ya usafirishaji haramu wa binaadamu na namna ya kuwalinda waathirika katika kongamano la vyuo vikuu la masuala ya msaada wa kisheria lililofanyika ukumbi wa Aboud Jumbe Tunguu Zanzibar ikiwa ni shamrashamra za maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria inayofikia kilele juni 28.
Kamishna wa kinga, tiba na marekebisho ya Tabia kutoka Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya Zanzibar Juma Abdul-Rahman Zidikheri akiwasilisha mada ya athari za dawa za kulevya kwa vijana katika kongamano la vyuo vikuu la masuala ya msaada wa kisheria lililofanyika ukumbi wa Aboud Jumbe Tunguu Zanzibar ikiwa ni shamrashamra za maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria, inayofikia kilele juni 28.
Mkuu wa Divisheni ya elimu na mafunzo- idara ya katiba na msaada wa kisheria Ali Haji Hassan akiwasilisha mada ya dhana ya msaada wa kisheria katika kongamano la vyuo vikuu la masuala ya msaada wa kisheria lililofanyika ukumbi wa Aboud Jumbe Tunguu Zanzibar ikiwa ni shamrashamra za maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria inayofikia kilele juni 28.

Mwanafunzi wa kada ya Sheria Chuo Kikuu cha Zanzibar ZU Omar Mustafa akichangia katika kongamano la vyuo vikuu la masuala ya msaada wa kisheria lililofanyika ukumbi wa Aboud Jumbe Tunguu Zanzibar ikiwa ni shamrashamra za maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria inayofikia kilele juni 28.
Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Abdulrahman Al-Sumait Ali Abdalla Sleiman akichangia katika kongamano la vyuo vikuu la masuala ya msaada wa kisheria lililofanyika ukumbi wa Aboud Jumbe Tunguu Zanzibar ikiwa ni shamrashamra za maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria inayofikia kilele juni 28.
Mwanafunzi wa kada ya Sheria Chuo Kikuu cha Zanzibar ZU ambae pia ni mtoa huduma za msaada wa kisheria chuoni hapo akichangia katika kongamano la vyuo vikuu la masuala ya msaada wa kisheria lililofanyika ukumbi wa Aboud Jumbe Tunguu Zanzibar ikiwa ni shamrashamra za maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria inayofikia kilele juni 28.


Na Fauzia Mussa, Maelezo 

Jaji wa Mahkama Kuu, Zanzibar Ibrahim Mzee Ibrahim amewataka wanajamii kuvitumia vituo vya msaada wa kisheria katika maeneo yao ili kupunguza gharama na kufuata huduma hiyo masafa ya mbali.

Akifungua Kongamano la vyuo vikuu la masuala ya msaada wa kisheria huko katika Ukumbi wa Aboud Jumbe Tunguu Zanzibar amesema lengo la Serikali kuanzisha vituo hivyo ni kuwaondoshea usumbufu huo na kuitaka jamii kuvitumia ipasavyo ili kufikia malengo yaliokusudiwa.

“Kabla ya kuwepo Wasaidizi wa Sheria katika jamii Watu wengi walikosa msaada wa kisheria jambo ambalo lilipelekea kukosa haki zao.” Alisema Jaji Ibrahim.

Amesema Msaada wa kisheria ni muhimu sana katika jamii kwani baadhi ya watu hawana uwezo wa kulipia Mawakili hivyo msaada wa kisheria utawajengea ujasiri wa kupambania haki hizo.

Aidha ameipongeza idara ya katiba na msaada wa kisheria kuandaa kongamano hilo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu ambapo litasaidia kuhamasisha upatikanaji wa huduma katika ngazi ya jamii na vyuo vikuu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Idara ya Katiba na msaada wa kisheria Zanzibar Hanifa Ramadhan Said amesema madhumuni ya Kongamano hilo ni kuwajengea uzalendo, kujitolea na kuisaidia jamii kupitia msaada wa kisheria.

Aidha amewataka Wanafunzi hao kuwaunga mkono katika shughuli mbalimbali zilizoandaliwa na Idara hiyo katika wiki ya msaada wa kisheria hadi kufikia kilele chake juni 28.

Hata hivyo amewashukuru wadau wa maendeleo wakiwemo UNDP na LSF kwa kuwaunga mkono na kuhakikisha jamii inapata haki zao kupitia msaada wa kisheria.

Mapema akitoa salamu za shirika la maendeleo la umoja wa mataifa UNDP Mratibu na mshauri wa program za utawala bora Godfrey Mulisa amesema shirika hilo litaendelea kuisaidia Serikali kupitia idara ya katiba na msaada wa kisheria katika mambo mbalimbali ikiwemo kutoa elimu ya msaada wa kisheria ili Wananchi wapate stahiki zao.

“haki ya kupata msaada wa kisheria ni ya kila mtu hivyo niwaombe muwafikie watoa huduma za msaada wa kisheria waliopo katika maeneo ili mupate haki zenu”. alisema Mwakilishi huyo.

Mkuu wa Skuli ya sheria Dk. Ali Ahmed Uki na Kaimu Mkuu wa kitivo cha sheria cha chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU) Dk. Sikujua Omar Hamdan wamesema uwaepo kwa Vituo vya msaada wa kisheria vyuoni kunasaidia kujenga weledi na uzowefu kwa wanafunzi wa kada ya sharia kuweza kuisoma kwa vitendo fani hiyo.

Aidha amesema hali hiyo pia itaweza kuwajengea moyo wa kuitumika jamii kwa kujitolea hata baada ya kumaliza masomo.

Hata hivyo amewataka Wanafunzi wanaotoa msaada wa kisheria chuoni wasivunjike moyo na pia ni sehemu ya mazoezi ya fani hiyo.

“Kazi hii ni nzito na ya kujitolea hivyo tusichoke ili kuisaidia jamii kupata haki zao.” Walisema.

Jumla ya mada tatu (3) zilijadiliwa katika kongamano hilo, ikiwemo dhana ya msaada wa kisheria, athari za dawa za kulevya kwa vijana na usafirishaji haramu wa binaadamu na namna ya kuwalinda waathirika ambapo limewashirikisha Wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali vya Zanzibar ikiwemo SUZA, IPA, AL- SUMAIT na ZU.

No comments: