Tuesday, June 25, 2024

SERIKALI YASITISHA ZOEZI LA UKAGUZI WA RISITI SOKO LA KARIAKOO


Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akieleza nia njema ya Serikali katika kuhakikisha kunakuwa na mazingira bora ya ufanyaji biashara nchini, wakati wa kikao kati ya Viongozi wa Wafanyabiashara Tanzania, Viongozi wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo na Taasisi zinazosimamia masuala ya wafanyabiashara, jijini Dodoma. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Jenista Mhagama.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (katikati), akitoa maazimio ya kikao kati ya Viongozi wa Wafanyabiashara Tanzania, Viongozi wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo na Taasisi zinazosimamia masuala ya wafanyabiashara, kikao ambacho kiliitishwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), na kulia ni Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo, Bw. Martin Mbwana.


Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akieleza namna Serikali ilivyo sikivu na inaendelea kutatua kero za wafanyabiashara nchini, wakati wa kikao kati ya Viongozi wa Wafanyabiashara Tanzania, Viongozi wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo na Taasisi zinazosimamia masuala ya wafanyabiashara, kikao ambacho kiliitishwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), jijini Dodoma. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (kushoto) na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Alphayo Kidata, wakifuatilia kwa umakini mjadala kati ya Serikali na viongozi wa Wafanyabiashara wa Kariakoo, jijini Dodoma.


Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Alphayo Kidata, akieleza kuhusu kusitisha kwa zoezi la ukaguzi wa risiti za Kielekroniki (EFD) na ritani za Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), iliyokuwa ikifanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kupitia mkoa wa kikodi wa Kariakoo, Jijini Dar es Salaam, wakati wa kikao kati ya Viongozi wa Wafanyabiashara Tanzania, Viongozi wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo na Taasisi zinazosimamia masuala ya wafanyabiashara, kikao ambacho kiliitishwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), jijini Dodoma.




Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, akieleza jitihada za Serikali katika kutatua changamoto za Wafanyabiashara wakati wa kikao na viongozi wa wafanyabiashara wa Kariakoo, jijini Dodoma

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (wa pili kushoto) na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakizungumza na Viongozi wa wafanyabiashara baada ya kumalizika kwa kikao kati yao jijini Dodoma, ambapo Serikali imeridhia kusitisha zoezi la ukaguzi wa risiti za Kielekroniki (EFD) na ritani za kodi (VAT), iliyokuwa ikifanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kupitia mkoa wa kikodi wa Kariakoo, Jijini Dar es Salaam, wakati ukiandaliwa utaratibu mzuri wa utekelezaji wa suala hilo katika Soko Kuu la Kimataifa la Kariakoo.



Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (wa pili kushoto) na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakizungumza na Viongozi wa wafanyabiashara baada ya kumalizika kwa kikao kati yao jijini Dodoma, ambapo Serikali imeridhia kusitisha zoezi la ukaguzi wa risiti za Kielekroniki (EFD) na ritani za kodi (VAT), iliyokuwa ikifanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kupitia mkoa wa kikodi wa Kariakoo, Jijini Dar es Salaam, wakati ukiandaliwa utaratibu mzuri wa utekelezaji wa suala hilo katika Soko Kuu la Kimataifa la Kariakoo.


Makamu wa rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara, Bw. Boniface Ndengo, akiipongeza Serikali kwa uamuzi wa kukutana na viongozi wa wafanyabiashara ili kutatua changamoto za wafanyabiashara nchini, wakati wa kikao kati ya Viongozi wa Wafanyabiashara Tanzania, Viongozi wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo na Taasisi zinazosimamia masuala ya wafanyabiashara, kikao ambacho kiliitishwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), jijini Dodoma.

Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Taifa, Bw. Hamisi Livembe, akiipongeza Serikali kwa uamuzi wa kusitisha kwa zoezi la ukaguzi wa risiti za Kielekroniki (EFD) na ritani za kodi (VAT), iliyokuwa ikifanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kupitia mkoa wa kikodi wa Kariakoo, Jijini Dar es Salaam, wakati wa kikao kati ya Viongozi wa Wafanyabiashara Tanzania, Viongozi wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo na Taasisi zinazosimamia masuala ya wafanyabiashara, kikao ambacho kiliitishwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo, Bw. Martin Mbwana, akieleza changamaoto mbaoimbali za wafanyabiashara wa Soko hilo ikiwemo ya zoezi la ukaguzi wa risiti za Kielekroniki (EFD) na ritani za kodi (VAT), iliyokuwa ikifanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kupitia mkoa wa kikodi wa Kariakoo, Jijini Dar es Salaam, ambalo Serikali imelisitisha, wakati wa mazungumzo kati ya Wafanyabiashara na Serikali, jijini Dodoma.



Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Eliezer Felesh, akieleza umuhimu wa wafanyabiashara nchini na namba ambavyo inashughulikia na kurekebisha sheria mbalimbali za masuala ya kodi, wakati wa kikao kati ya Viongozi wa Wafanyabiashara Tanzania, Viongozi wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo na Taasisi zinazosimamia masuala ya wafanyabiashara, kikao ambacho kiliitishwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), jijini Dodoma.

No comments: