Sunday, August 4, 2024

MAKAMU WA RAIS ASAFIRI KWA TRENI KUSHIRIKI YANGA DAY



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango wakiwasili katika Stesheni ya Treni ya Jijini Dar es Salaam mara baada ya kusafiri kutoka Dodoma kuelekea Dar es salaam kwa kutumia Usafiri wa Treni ya Kisasa ya Umeme inayotumia Reli ya Kisasa (SGR). Tarehe 04 Agosti 2024.

Makamu wa Rais amesafiri kuelekea Jijini Dar es Salaam ambapo anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Tamasha la Klabu ya Yanga la kilele cha Wiki ya Mwananchi litakalofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.





No comments: