Sunday, August 4, 2024

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MSAPINDUZI MHE.DK.HUSSEIN MWINYI AMEFUNGUA MONESHO YA SABA YA KILIMO NANENANE VIWANJA VYA KIZIMBANI


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Hodhi la Kuhifadhia Maji katika viwanja vya Maonesho ya Kilimo Kizimbani Wilaya ya Magharibi “A”Unguja wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Kilimo ya Nanenane uliofanyika leo 3-8-2024,na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Muwakilishi wa Taasisi ya AATIF Rashid Ali Rashid, kuhusiana na Kilimo cha mbogamboga wakati akitembelea Maonesho ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Kizimbani Wilaya ya Magharibi “A” Unguja, aliyoyafungua leo 3-8-2024 katika viwanja hivyo na (kulia kwa Rais) Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo ,Umwagiliaji,Maliasili na Mifugo Ndg.Ali Khamis na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrissa Kitwana Mustafa
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Afisa Mifugo Muandamizi Bi. Zehra Karim Zam, akitowa maelezo ya ufugaji wa Kuku, wakati akitembelea banda la maonesho la Idara ya Maendeleo ya Mifugo Zanzibar, katika maonesho ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Kizimbani Wilaya ya Magharibi “A” Unguja. aliyoyafungua leo 3-8-2024 katika viwnja hivyo

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa amemshika Kaa wakati akipata maelezo ufugaji wa Kaa kutoka kwa Kamishna wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Khamis Bakar Khamis, wakati akitembelea banda la maonesho la Chuo cha Mafunzo Zanzibar, katika viwanja vya Kizimbani Wilaya ya Magharibi “A” Unguja, wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Kilimo ya Nane Nane aliyoyafungua leo 3-8-2024 katika viwanja hivyo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia kuweka jiwe la msingi la Kituo cha Biashara ya Maziwa katika viwanja vya Maonesho ya Nane Nane Kizimbani Wilaya ya Magharibi “A” Unguja, wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Kilimo ya Nanenane, aliyoyafungua leo 3-8-2024, katika viwanja hivyo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akitembelea Maonesho ya Kilimo ya Nane Nane katika viwanja vya Kizimbani Wilaya ya Magharibi “A”Unguja, wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo uliofanyika leo 3-8-2024

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo ya Kitaalamu ya ukaushaji wa Samaki kutoka kwa Sajenti Eliyas Lumalijo, wakati akitembelea banda la maonesho la Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar (JKU) katika viwanja vya maonesho Kizimbani Wilaya ya Magharibi “A” Unguja leo 3-8-2024, wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo.


No comments: