Thursday, October 3, 2024

WAZIRI KIJAJI AKAGUA MITO TEGETA, SEGEREA ATOA MAELEKEZO


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akikagua athari za kimazingira katika Mto Segerea Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya tarehe 02 Oktoba, 2024 akiwa ameambatana na Na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis na watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akikagua athari za kimazingira katika Mto Segerea Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya tarehe 02 Oktoba, 2024 akiwa ameambatana na Na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis na watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Toba Nguvila alipofika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa kabla ya kuanza ziara ya kukagua athari za mazingira katika Mto Segerea na Mto Tegeta mkoani humo. Kulia kwa ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ameielekeza Ofisi ya Bonde la Mto la Wami Ruvu kidakio cha Pwani kutoa vibali vya kusafisha Mto Tegeta ili kulinda mazingira na kupunguza athari kwa watu na mali zao pamoja na miundombinu ya umma.

Ametoa maelekezo hayo alipotembelea Mto Tegeta wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam tarehe 02 Oktoba, 2024 na kujionea hali halisi ya mto na uharibifu wa mazingira unaofanywa na wakazi wa maeneo hayo ikiwemo utupaji wa taka katika mto huo.

Mhe. Dkt. Kijaji amesema ni lazima kutafuta suluhisho la kunusuru kingo za mito na kupunguza athari za mafuriko na kusisitiza wale wote walioomba vibali wapewe kwa ajili ya kusafisha mto huo.

Akijibu pendekezo la Mbunge wa Kawe Mhe. Askofu Dkt. Josephat Gwajima la kutaka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuitisha kikao cha wadau wote wanaochimba mchanga kwa ajili ya kuwaelimisha kuhusu utunzaji na usafishaji wa mito.

Hiyo, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ameiagiza NEMC kwa kushirikiana na Kikosi Kazi kuandaa kikao hicho na kuwataka wenyeviti waliopo kwenye maeneo ya mito yote kufika na wawakilishi wa wananchi.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Semesi amesema Baraza limepokea maelekezo ya Waziri na kwa kushirikiana na Mhe. Dkt. Gwajima pamoja na Kikosi kazi kikao cha wadau kitafanyika kwa ajili ya kupata mawazo yao na kuwaelimisha juu ya Utunzaji na usafishaji wa mito hiyo.

Katika ziara hiyo Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji aliyeambatana na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis pia alitembelea Mto Segerea wilayani Ilala na kushuhudia kupanuka kwa kingo za mto huo na kuagiza usafishaji wa mto huo uanze mara moja ili kunusuru mazingira.

No comments: