Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi akizungumza kuhusu kazi pamoja na namna Mamlaka hiyo inavyosimamia Usafiri wa Anga wakati wa utunukishaji zawadi na Tuzo kwa wanafunzi Bora wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) yenye lengo la kujenga ushindani na kuhamasisha juhudi katika masomo baina ya wanafunzi.
Baadhi ya Wadau mbalimbali kutoka Taasisi na Makampuni pamoja na Wanafunzi wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) wakifuatila zoezi la utoaji wa Tuzo likiwa na lengo la kujenga ushindani na kuhamasisha juhudi katika masomo baina ya wanafunzi.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Daniel Mushi akitembelea mabanda ya wabunifu kutoka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) wakati wa kugawa tuzo za wanafunzi bora ikiwa na lengo la kujenga ushindani na kuhamasisha juhudi katika masomo baina ya wanafunzi.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Daniel Mushi akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Taasisi pamoja na kampuni mbalimbali wakati utunukishaji zawadi na Tuzo kwa wanafunzi Bora wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw.Salim Msangi amesema taasisi yake itafanya mashirikiano na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam(DIT), ili kupata watalaam katika Usafiri wa Anga nchini.
Mkurugenzi Mkuu Mkuu Msangi ameyasema hayo Desemba 4,2024 wakati akitoa salamu za TCAA katika hafla ya kutoa tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika taaluma na ubunifu wa teknolojia chuoni hapo jijini Dar es Salaam, na kuongeza kuwa amefurahishwa sana kwa kupata fursa ya kutembelea, kujifunza na kujionea mambo mazuri ya DIT.
Amesema atatoa nafasi kwa wataalam wake kutembelea DIT na kuangalia uwezekano huo wa kuangalia maeneo ya mashirikiano.
Awali Mkurugenzi Mkuu Msangi aliieleza hadhira ya DIT kuhusu TCAA na majukumu yake ikiwemo ya Udhibiti na Ukaguzi wa sekta ya usafiri wa Anga nchini.
Na kuwakumbusha kwamba Mamlaka sio tu ina jukumu ka usimamizi na kutekeleza sheria za nchi bali pia ina jukumu la kuhakikisha soko la Usafiri wa Anga linakua pamoja na kuzingatia ukuaji wa teknolojia.
Bw. Msangi aliwakumbusha kuhusu hatua ya TCAA kutoa cheti kwa Kampuni ya AAL yenye Makao yake Makuu mkoani Morogoro ambayo sasa inaunda Ndege zake hapa nchini.
Bw. Msangi ameipongeza DIT kwa kutoa tuzo za kitaaluma na ubunifu wa teknolojia na kuongeza kuwa wanayoyafanya yanaweza kuwa na msaada katika maeneo ya Usafiri wa Anga.
Hafla hiyo ya utoaji tuzo iliongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Daniel Mushi akishuhudiwa na wanafunzi pamoja na wadau mbalimbali akiwemo Mkuu wa Chuo cha DIT Prof.Preksedis Ndomba.
No comments:
Post a Comment