Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiongoza vikao vya bodi ya taasisi hiyo Jijini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ni Mheshimiwa Reem Al Hashimy, Waziri anayeshughulikia Ushirikiano wa Kimataifa wa Umoja wa Falme za Kiarabu.Kushoto kwa Mheshimiwa Dkt Kikwete ni Bi. Christine Hogan, Naibu Mwenyekiti wa Bodi ya GPE.
Rais Mstaafu wa Tanzania Mhe.Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ni Mheshimiwa Prof. Nasser Al Aqeeli, Naibu Waziri wa Elimu wa Ufalme wa Saudi Arabia. Kushoto kwa Mheshimiwa ni Naibu Mwenyekiti wa Bodi ya GPE Christine Hogan na Mheshimiwa Waziri Reem Al Hashimy, Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Umoja wa Falme za Kiarabu.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Elimu la Kimataifa (GPE), Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa na Mheshimiwa Prof. Nasser Al Aqeeli, Naibu Waziri wa Elimu wa Ufalme wa Saudi Arabia. Kushoto kwa Mheshimiwa ni Naibu Mwenyekiti wa Bodi ya GPE Christine Hogan na Mheshimiwa Waziri Reem Al Hashimy, Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Umoja wa Falme za Kiarabu
PICHA NA OFISI YA RAIS MSTAAFU
Na Mwandishi Maalumu
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Elimu la Kimataifa (GPE), anaongoza vikao vya bodi ya taasisi hiyo jana na leo Jijini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
Vikao hivyo vilifunguliwa rasmi jana na Mhe. Reem Al Hashimy, Waziri wa Nchi wa UAE anayeshughulikia Ushirikiano wa Kimataifa. Umoja wa Falme za Kiarabu umekuwa mshirika muhimu wa GPE kwa miaka kadhaa.
Vikao hivyo vinawakutanisha wajumbe wa bodi wakilisha wa nchi mbalimbali, mashirika ya kimataifa, na vyama vya kiraia kutoka pande zote za dunia.
Miongoni mwa wahudhuriaji mashuhuri alikuwa Mhe. Prof. Nasser Al Aqeeli, Naibu Waziri wa Elimu wa Saudi Arabia, aliyeelezea dhamira ya Ufalme wa Saudi Arabia kuendelea kushirikiana na GPE katika kutatua changamoto za elimu msingi (chekechea, elimu ya msingi, na sekondari) katika nchi zinazoendelea.
GPEni mpango wa kimataifa unaolenga kuboresha elimu katika nchi zinazoendelea, hasa kwa watoto waliotengwa au wanaokosa fursa.
Ukiwa imeanzishwa mwaka 2002, GPE inasaidia elimu ya awali, msingi, na sekondari kwa kuzingatia usawa, ujumuishi, na ubora wa masomo.
Shirika hili pia huhamasisha rasilimali, kushirikiana na serikali, mashirika ya kiraia, na taasisi za kimataifa, na hutoa ruzuku zinazolenga matokeo.
Kwa kuimarisha mifumo ya elimu, GPE linaendana na Lengo la Maendeleo Endelevu 4, kuhakikisha elimu jumuishi na bora.
Tayari limebadilisha maisha ya mamilioni ya watoto katika nchi zaidi ya 90 kwa kuwapa fursa ya elimu bora na maendeleo endelevu.
No comments:
Post a Comment