ANGALIA LIVE NEWS

Monday, December 9, 2024

RAIS WA ZANZIBAR DK. HUSSEUIN MWINYI AJUMUIKA NA WANANCHI NA VIKUNDI VYA MAZOEZI YA VIUNGO ZANZIBAR KATIKA MATEMBEZI YA AFYA ZANZIBAR


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakijumuika na Wanavikundi vya mazoezi katika Matembezi ya Afya Zanzibar “ Chagua Mazoezi kuwa Sehemu ya Maisha Yako” yaliyoazia katika viwanja vya Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B”Unguja na kumalizikia katika Uwanja wa Mao Zedung Wilaya ya Mjini Unguja leo 8-12-2024 (kulia kwa Rais) Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hassan Khamis Hafidh.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi (kushoto kwake) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa ,wakijumuika na Wanavikundi vya mazoezi Zanzibar katika Matembezi ya Afya Zanzibar “ Chagua Mazoezi kuwa Sehemu ya Maisha Yako” yaliyoazia katika viwanja vya Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B”Unguja na kumalizikia katika Uwanja wa Mao Zedung Wilaya ya Mjini Unguja na (kulia kwa Rais) Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hassan Khamis Hafidh, yaliyofanyika leo 8-12-2024
WASHIRIKI wa Matembezi ya Afya Zanzibar “ Chagua Mazoezi kuwa Sehemu ya Maisha Yako” kutoka Vikundi mbalimbali vya mazoezi Zanzibar wakimalizia matembezi hayo katika Uwanja wa Mao Zedung Wilaya ya Mjini Unugja, yaliyoazia katika viwanja vya Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 8-12-2024
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kitengo cha Damu Salama Zanzibar Dkt. Masoud Ali Masoud, wakati akitembelea maonesho ya Afya Zanzibar, baada ya kumaliza matembezi ya Afya Zanzibar “Chagua Mazoezi kuwa Sehemu ya Maisha Yako” katika uwanja wa Mao Zedung Wilaya ya Mjini Unguja leo 8-12-2024 na (kulia kwa Rais) Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui na (kushoto kwa Rais) Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hassan Khamis Hafidh
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Programu ya Kumaliza Malaria Zanzibar. Shija Joseph Shija, wakati akitembelea maonesho ya Afya Zanzibar, baada ya kumaliza matembezi ya Afya Zanzibar “Chagua Mazoezi kuwa Sehemu ya Maisha Yako” katika uwanja wa Mao Zedung Wilaya ya Mjini Unguja leo 8-12-2024 na (kulia kwa Rais) Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui na (kushoto kwa Rais) Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hassan Khamis Hafidh
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Msaidizi Meneja Kitengo cha Maradhi Yasioambukiza (NCD) Zuhura Saleh Amour ar Dkt. Shija Joseph Shija, wakati akitembelea maonesho ya Afya Zanzibar, baada ya kumaliza matembezi ya Afya Zanzibar “Chagua Mazoezi kuwa Sehemu ya Maisha Yako” katika uwanja wa Mao Zedung Wilaya ya Mjini Unguja leo 8-12-2024 na (kulia kwa Rais) Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui na (kushoto kwa Rais) Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hassan Khamis Hafidh.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwahutubia Wanamichezo wa Vikundi vya Mazoezi ya Viungo Zanzibar, baada ya kumalizika kwa Matembezi ya Afya Zanzibar “Chagua Mazoezi kuwa Sehemu ya Maisha Yako” yaliyofanyika leo 8-12-2024, katika viwanja vya Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja na kumalizika katika Uwanja wa Mao Zedung Wilaya ya Mjini Unguja.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwahutubia Wanamichezo wa Vikundi vya Mazoezi ya Viungo Zanzibar, baada ya kumalizika kwa Matembezi ya Afya Zanzibar “Chagua Mazoezi kuwa Sehemu ya Maisha Yako” yaliyofanyika leo 8-12-2024, katika viwanja vya Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja na kumalizika katika Uwanja wa Mao Zedung Wilaya ya Mjini Unguja.
WANAMICHEZO wa Vikundi vya Mazoezi ya Viungo Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia baada ya kumalizika kwa Matembezi ya Afya Zanzibar “Chagua Mazoezi kuwa Sehemu ya Maisha Yako” yaliyoazia katika viwanja vya Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja na kumalizikia katika viwanja vya Mao Zedung Wilaya ya Mjini Unguja leo 8-12-2024
WANAMICHEZO wa Vikundi vya Mazoezi ya Viungo Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia baada ya kumalizika kwa Matembezi ya Afya Zanzibar “Chagua Mazoezi kuwa Sehemu ya Maisha Yako” yaliyoazia katika viwanja vya Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja na kumalizikia katika viwanja vya Mao Zedung Wilaya ya Mjini Unguja leo 8-12-2024.
WANAMICHEZO wa Vikundi vya Mazoezi ya Viungo Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia baada ya kumalizika kwa Matembezi ya Afya Zanzibar “Chagua Mazoezi kuwa Sehemu ya Maisha Yako” yaliyoazia katika viwanja vya Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja na kumalizikia katika viwanja vya Mao Zedung Wilaya ya Mjini Unguja leo 8-12-2024
MKE wa Rais wa Zanzibar na Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mama Marian Mwinyi (kushoto kwake) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi,akikabidhiwa TUZO maalum ya kuthamini mchango wake katika Sekta ya Afya Zanzibar, akikabidhiwa na Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui, baada ya kumalizika kwa Matembezi ya Afya Zanzibar “Chagua Mazoezi kuwa Sehemu ya Maisha Yako”yaliyomalizikia katika Viwanja vya Mao Zedung Wilaya ya Mjini Unguja leo 8-12-2024
MKE wa Rais wa Zanzibar na Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mama Marian Mwinyi (kushoto kwake) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi,akikabidhiwa TUZO maalum ya kuthamini mchango wake katika Sekta ya Afya Zanzibar, akikabidhiwa na Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui, baada ya kumalizika kwa Matembezi ya Afya Zanzibar “Chagua Mazoezi kuwa Sehemu ya Maisha Yako”yaliyomalizikia katika Viwanja vya Mao Zedung Wilaya ya Mjini Unguja leo 8-12-2024.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuchukua juhudi maalum kuhakikisha inapunguza kasi ya ongezeko la Maradhi yasiombukiza hapa nchini

Rais Dk,Mwinyi ametoa tamko hilo alipozungumza baada ya Kuongoza matembezi ya Afya yalioandaliwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Taasisi ya Pharm Access ikiwa ni kampeni maalum ya kudhibiti Maradhi yasioambukiza kwa jamii yalioanzia Kiembe Samaki kwa Boutros hadi Uwanja Mao Tse Tung Wilaya ya Mjini.

Rais Dk,Minyi amefahamisha kuwa Tafiti zimeonesha kuwa Mazoezi yanasaidia kwa kiasi kikubwa kujenga Afya ya Mwili ,afya ya akili na kuondosha Msongo wa Mawazo na kusisitiza jamii kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi kila siku

Aidha Dk, Mwinyi ameeleza kuwa Takwimu za Wizara ya Afya zimeeleza kuwa kuna Ongezeko la Maradhi Yasioambukiza kwa kiwango kikubwa ikwemo Kisukari, Presha , Uzito na Unene uliopitiliza na shinikizo la damu kunakosababishwa na watu wengi kutofanya mazoezi.

Rais Dk, Mwinyi ameeleza kuwa kutofanya Mazoezi kwa Wananchi walio wengi kunarejesha nyuma juhudi za Serikali za kudhibiti Maradhi hayo na kupunguza kasi ya kuleta Maendeleo.

Aidha Rais Dk,Mwinyi amesisitiza kuwa Serikali imeendelea kushirikiana na taasisi za Afya kutoa Elimu na kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa kufanya mazoezi kwa ajili ya kuimarisha afya zao.

Amefahamisha kuwa Mazoezi yanasaidia kuondoa Msongo wa Mawazo , kuimarisha Usingizi na kuleta furaha.

Ameeleza kuwa wizara ya Afya imeendelea kutoa matibabu bora katika Vituo 60 viliopo Unguja na Pemba na Kuwasisitiza wananchi kuvitumia Vituo hivyo kupata ushauri wa Kitaalamu wa afya zao.

Rais Dk, Mwinyi ametoa wito kwa kila mmoja kuchukua hatua ya kupunguza Mafuta na matumizi ya vyakula vya wanga kukabiliana na maradhi hayo.

Ameeleza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Taasisi Gez Health Initiative inaendelea kutoa Elimu ,kufanya Uchunguzi wa Awali wa Maradhi ya Saratani kupitia Mradi wa miaka mitano wa kudhibiti Saratani pamoja na Ujenzi wa kituo cha Umahiri cha Saratani hapa Zanzibar.

Rais Dk, Mwinyi ameshauri kuendelezwa na kupangiwa Utaratibu mzuri wa Matembezi ya pamoja na mazoezi .

Aidha Amezipongeza Taasisi mbalimbali zinazoshirikiana na Serikali kufanikisha juhudi za Kudhibiti Maradhi yasioambukiza

Waziri wa Afya Nassor Ahmed Mazrui amesema Dhamira ya Serikali ni kuona wananchi wote wana afya njema na kutambua kuwa suala la kufanya mazoezi sio anasa na Wizara najiandaa kuwa na siku maalum ya mazoezi kila mwezi.

Ametoa rai kwa Taasisi za Umma na binafsi kuandaa utaratibu wa kuwa na siku maalum ya kufanya mazoezi.

Mkurugenzi wa Pharm Access Kheri Marwa ameeleza kuwa tatizo la Maradhi yasioambukiza ni kubwa duniani kote hivyo juhudi kubwa zinapaswa kuchukuliwa kuhamasisha ufanyaji wa mazoezi kwa wananchi.

Matembezi hayo ya Afya yamebeba Kaulimbiu inayosema "Chagua Mazoezi kuwa Sehemu ya Maisha ".

No comments: