Mahakama ya Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya, imemuhukumu Kijana aitwaye Owen Uswege Mwambera (20), Mkazi wa matenki border kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kupatikana pamoja na kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi zenye uzito wa zaidi ya kilogramu 7.
Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya leo February 20, 2025 imesema hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Andrew Njau - SRM na Mwendesha mashitaka wa Jeshi la Polisi Mkaguzi Msaidizi Bihemo Dawa Mayengela February 17, 2025 katika Mahakama ya Wilaya ya Kyela kwa mujibu wa kifungu cha 15A kifungu kidogo cha kwanza na cha pili (c) cha sheria ya Udhibiti na Usimamizi wa Dawa za Kulevya sura ya 95 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.
Mshitakiwa Owen anadaiwa kutenda kosa hilo July 12, 2024 kwa kubeba dawa hizo za kulevya zenye uzito wa Kilogramu 7.06 ambapo alikamatwa na Polisi katika eneo la geti la ushuru wa mazao maarufu Mafiga Wilayani Kyela akiwa katika harakati za kusafiri nazo kuelekea Mbeya Mjini.

No comments:
Post a Comment