Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali Itaendelea na Mikakati Mbalimbali kuhakikisha inawekeza kwa ajili ya Utekelezaji wa Miradi Mikubwa zaidi ya Maendeleo hapa nchini .
Rais Dkt, Mwinyi ametoa tamko hilo alipozindua Hatifungani ya ZANZIBAR SUKUK, VIwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.
Amefahamisha kuwa Serikali imeamua kwa makusudi kuwa na Utaratibu wa Hati Fungani kuwa njia rasmi ya kuyafikia Maendeleo Endelevu hivyo SUKUK itaenda Kufanikisha azma hiyo.
Dkt,Mwinyi ameeleza kuwa Serikali imepanga kutekeleza Miradi mingi katika Muda Mfupi Ujao hivyo kuwepo kwa ZANZIBAR SUKUK kutaipa Serikali Uwezo na Uhakika wa kupata Fedha za Utekelezaji wa Miradi hiyo.
Dkt, Mwinyi amebainisha kuwa Nchi nyingi Zilizoendelea Duniani zimefanikiwa kwa kupitia Mfumo huo wa SUKUK unaozingatia Misingi ya Sharia.
Rais Dkt, Mwinyi ameeleza kuwa lengo ni kuimarisha Uwezo wa Zanzibar Kiuchumi na Kuwasisitiza Wananchi ,Wadau na Taasisi za Umma na Binafsi kuchangamkia fursa hiyo Inayompa mdau Faida ya Asilimia 10.5 kila Mwaka kuwa njia muhimu ya kujiimarisha Kiuchumi.
Rais Dkt,Mwinyi amefahamisha kuwa Mageuzi Makubwa ya Kiuchumi Yanayofanyika hivi sasa hapa nchini yanafanyika kufuatia Kiu kubwa walionayo Wananch na Uhitaji wa Nchi katika Maendeleo.
Rais Dkt, Mwinyi ameeleza kuwa Mafanikio ya hatua hiyo yanahitaji Ushiriki wa Wananchi wengi watakaonunua Hatifungani za ZANZIBAR SUKUK na kuwahakikishia kuwa ipo katika Hali nzuri.
Rais Dkt, Mwinyi amesisitiza kuwa Utaratibu huo Utaweka Usalama na Utulivu wa Sekta ya Kifedha Nchini.
Rais DKt Mwinyi ametumia Fursa hiyo kukanusha Taarifa Potofu zinazosambazwa na baadhi ya Wanasiasa wa Upinzani Kuwa Serikali inakusudia Kuiuza Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ.
Ameeleza kuwa Kinachofanyika ni kuijengea Uwezo Benki hiyo ili Iwe na Mtaji Mkubwa zaidi wa kuikopesha Serikali kutekeleza Miradi Mikubwa ya Maendeleo na kuwataka Wananchi kupuuza taarifa hizo.
VIONGOZI mbalimbali wa Serikali na Wageni waalikwa wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia katika hafla ya Uzinduzi wa Zanzibar SUKUK, uliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar leo 22-2-2025.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizindua App ya Zanzibar SUKUK,wakati wa hafla ya uzinduzi huo uliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar leo 22-2-2025, (kushoto kwa Rais ) Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Arafat A.Haji na (kulia kwa Rais) CPA Juma Amour Mohammed.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizindua kitabu cha muongozi wa Zanzibar SUKUK,wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar leo 22-2-2025, (kushoto) Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Dkt.Saada Mkuya Salum
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizindua kitabu cha muongozi wa Zanzibar SUKUK,wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar leo 22-2-2025, na (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Dkt.Saada Mkuya Salum. na CPA.Juma Amour Mohammed na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla












No comments:
Post a Comment