Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akikata utepe kuashiria ufunguzi wa mradi wa uwekezaji wa Mgahawa, maduka na mini supermarket uliofanywa na Ndugu Abdullah Salim Turkey katika eneo la Barabara ya DT Bweleo Wilaya ya Maghari
Wawekezaji wa ndani wametakiwa kuendelea kubuni Miradi ya uwekezaji ili kusaidia upatikanaji wa huduma mbali mbali Nchini.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameyasema hayo katika Hafla ya Ufunguzi wa My home furniture, Mini market Pamoja na the garden restaurant Bweleo Wilaya ya Magharibi 'B'.
Amesema hatua iliyochukuliwa na muwekeza wa mradi huo Ndugu Abdallah Salim Turkey ni ya kizalendo ambayo inaakisi dhamira ya Serikali ya Awamu ya nane inayoongozaa na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi kuwekeza katika kuwasogea huduma Wananchi.
Makamu wa Pili wa Rais amesema dhamira ya uwepo wa Miradi ya uwekezaji Nchini ni kusaidia kuongezeka kwa Pato la Taifa ambalo litapelekea ongezeko la ukusanyaji wa Kodi itakayosaidia kuleta Maendeleo endelevu Nchini.
Mhe.Hemed amempongeza muwekezaji huyo kwa kuamua kuwekeza katika eneo hilo na kumuomba kuelekeza ajira kwa wakazi wa eneo hilo ili na wao waweze kunufaika na mradi huo.
Nae muwekezaji wa mradi huo Ndugu Abdullah Salim Turkey amemueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa uwekazqji alioufanya utawasaidia Wananchi wa Bweleo, Fumba na maeneo jirani pamoja na wageni wanaotalii kwa kujipatia bidhaa mbali mbali.
Ndugu Turkey amemuhakikisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa Mradi huo utazalisha ajira kwa vijana ili kuwakomboa na umasikini na kukuza Pato la Taifa.
Akimkaribisha Mgeni Rasmi Mbunge wa Jimbo la Mpendae Mhe. Tawfyq Salim Turkey amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa maelekezo yake yaliyopelekea kulifungua eneo la Fumba na maeneo jirani ambapo uwepo wa mradi huo utasaidia Wananchi kupata bidhaa mbali mbali na kukuza uchumi wa Zanzibar.
Uzinduzi wa mradi huo umeendana na Iftari iliyoandaliwa na Muwekezaji huyo iliyowakutanisha wadau wa maendeleo, wanafamilia na Wananchi wa maeneo hayo.
No comments:
Post a Comment