William Peter Kisaka pia ujulikana Kwa jina la William Kinyonga, alikuwa mpiga drumz wa zamani na mmoja wa waasisi wa bendi ya Simba Wanyika, bwana huyu amekuwa akiteseka na maradhi Nchini Kenya
William, kwa muda alikuwa akiishi maisha magumu ya kuokota vitu na kujikimu mitaani, ni ndugu wa Wilson Peter na George Peter, ambao walikuwa pamoja naye wakiwa wanamuziki mahiri nchini Kenya .kuanzia miaka ya 1970.
Kaka zake Wote wawili walisha fariki dunia miaka mingi iliyopita.
Kwa jitihada za bwana Geoffrey Mosira sasa hivi yupo katika.makazi ya wazee jijini NAIROBI
Kulikuwa na habari nyingi hapa Tanzania kuwa Kuna mpango wa kumleta nyumbani Kwa matibabu LAKINI jambo hilo halikufanyika
Kwa mujibu wa taarifa William amekuwa akikabiliwa na changamoto za afya ya akili.



No comments:
Post a Comment