Na: Mwandishi Wetu,
ZANZIBAR.
Tukio la Muziki, Utamaduni na Ubunifu, FuToPiA Zanzibar Msimu wa Pili, litafanyika Fumba Town, Unguja tarehe 8 na 9 Agosti, 2026.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa FuToPiA, Lorenz Herrman, amesema mwaka huu tamasha linarudi kubwa zaidi baada ya mwanzo mzuri mwaka jana.
“Tiketi zimeshaanza kuuzwa. Raia wa Tanzania Tsh 35,000, Afrika Mashariki Tsh 65,000, Kimataifa Tsh 130,000 na VIP Tsh 260,000,” amesema Herrman.
Tamasha linaloandaliwa na Busara Promotions litajumuisha muziki, sanaa, chakula, afya na soko la Kwetu Kwenu Market ikijumlisha pia Food Art Street, Afya Zone, Wonder Zone kwa watoto na michezo ya asili kwa Wazee.
![]() |
| Mkurugenzi wa FuToPiA, Lorenz Herrman |
Wasanii wanaotarajiwa ni DJ Joozey, DJ Zoro, Baba Kash, Sauti Marley, Ruth Mlawa, DJ LAG kutoka Afrika Kusini, Vania Ice kutoka Burundi na wengineo wakiwemo mataifa ya Mexico, Canada, Chile na kwingine.
Mitindo itakayopigwa ni Afro House, Singeli, Afro Pop na midundo ya asili.
Kutakuwa pia na usafiri wa mabasi maalum kutoka Stone Town na Uwanja wa Ndege wa Zanzibar.
Lengo la FuToPiA ni kuwakutanisha watu, kuwainua wabunifu na wajasiriamali na kuonesha Zanzibar ni zaidi ya fukwe.
Baadhi ya matukio na Wasanii watakaokuwepo Msimu wa pili wa FuToPiA Zanzibar Agosti 8-9.















No comments:
Post a Comment