ANGALIA LIVE NEWS
Wednesday, November 6, 2024
RAIS WA ZANZIBAR DKT. HUSSEIN MWINYI AMTEMBELEA BANDARI YA SHANGAI CHINA
MHE. MWINJUMA AAGIZA MAAFISA UTAMADUNI KUIMARISHA MATAMASHA YA UTAMADUNI
TANZANIA NA UGANDA ZAKUTANA KUJADILI UIMARISHAJI MPAKA WA KIMATAIFA
RC CHALAMILA AAGA MWILI WA JAJI KIPENGA MUSSA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, leo Novemba 04, 2024, ameungana na umati wa waombolezaji katika misa ya kuaga mwili wa Jaji Kipenka Msemembo Mussa katika Kanisa la Kiinjili la (KKKT) dayosisi ya mashirika ya pwani usharika wa wazo hill
RC Chalamila katika tukio hilo maalum aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Saad Mtambuka, Kamanda wa wa Polisi Kanda Maalum Jumanne Muliro, pamoja na majaji wengine, ambapo RC Chalamila amesihi kuishi kwa upendo na kuonesha ushirikiano kwa familia ya marehemu kwa kumuenzi Mzee Kipenka Mussa
DKT. MWAMBA ATETA NA UJUMBE KUTOKA EU
Kikao cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Timu ya Wataalamu kutoka Umoja wa Ulaya nchini iliyoongozwa na Mkuu wa Masuala ya Ushirikiano wa Umoja wa Ulaya nchini, Bw. Marc Stalmans, kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Katibu Mkuu, jijini Dodoma, ambacho kilijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Serikali na Umoja wa Ulaya na tathmini ya programu ya Neighbourhood Development International Cooperation Instrument (NDICI) na Multi-annual Indicative Programme 2021-2027 (MIP 2021-2027) kwa kipindi cha miaka minne ya utekelezaji, 2021-2024.
MLELE KUANZA KUTUMIA SHERIA NDOGO KUWABANA WATUPA TAKA HOVYO!
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mlele mkoani Katavi wameridhia kuanza kutumika kwa sheria ndogo za Halmashauri hiyo hasa kwa watu wasiozingatia suala la usafi katika maeneo yao ya makazi na biashara.
Azimio hilo limekuja kwa lengo la kudhibiti uchafu katika maeneo mbalimbali ya halmashauri hiyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo bwana Sudi Mbogo ametangaza uamuzi huo katika kikao cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/ 2025 ambapo alisema watu wamekuwa na tabia ya kutupa taka hadi ndani ya mitaro na kusababisha mitaro kuziba.
Sheria hiyo ndogo ya usafi wa mazingira katika halmashauri ya Mlele itamwajibisha kwa kulipa faini ya shilingi elfu hamsini mtu yeyote atakayebainika kuchafua mazingira.
Bwana Mbogo ameeleza kuwa licha ya elimu juu ya usafi kutolewa bado wananchi wamekuwa wakikaidi na kutupa taka hovyo.
“Kamati ya fedha, uongozi na mipango iliridhia menejiment kutumia Sheria ndogo ili kuwabana wakorofi wachache ili kuweka mji wetu wa Inyonga kwenye mazingira ya usafi” alisema.
William Lula ni diwani katika halmashauri ya Mlele, alisema madhara ya uchafu ni pamoja na kusababisha magonjwa ya milipuko katika jami.
Aliongeza kuwa magonjwa .hayo yatasababisha serikali kutumia fedha nyingi kutibu watu watakaokuwa wameugua.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Ilunde Martin Mgoloka alisema fmpango huo utasaidia kununua vitendea kazi vya usafi kutokana na edha zitakazopatikana katika faini hizo.
Baadhi ya wafanyabiashara wa Inyonga walipoulizwa kuhusiana na suala la usafi na kuanza kutumika kwa sheria ndogo waliunga mkono suala Hilo na kuongeza kuwa kwa kufanya hivyo mji wa Inyonga utakuwa wa kuvutia zaidi.
” Tumewekewa barabara za lami na TANROADS pamoja na mitaro mizuri sana iliyobaki ni kazi yetu kufanya mji wetu kuwa safi” alisema Luhanda Paul.
VITUO VYA TAARIFA NA MAARIFA VYATOA MAPENDEKEZO UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA
Tuesday, November 5, 2024
MENO YA TEMBO-SONGWE
UCHAGUZI WA URAIS MAREKANI 2024
KAMPUNI YA UCHIMBAJI DHAHABU YA BARRICK KUJENGA BARABARA YA KM 73.9 KIWANGO CHA LAMI
Imeelezwa kwamba Kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Barrick inaendelea na utekelezaji wa ujenzi wa Barabara ya Kahama hadi Bulyanhulu yenye urefu wa kilomita 73.9 kwa kiwango cha lami itakayogharimu kiasi shilingi zaidi ya bilioni 100.
Hayo yalielezwa hivi karibuni na Meneja wa Kampuni ya Barrick nchini Tanzania Melkiory Ngido wakati akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari kuhusu Mpango wa Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo yenye ubia na Serikali ya Tanzania.
Akielezea kuhusu faida zitakazopatikana pindi mradi huo utakapo kamilika , Ngido alieleza kuwa wananchi wa Wilaya ya Kahama watapata fursa ya kusafirisha na kushiriki maendeleo ya kiuchumi pamoja na kusafiri kwa wepesi katika kutafuta huduma muhimu.
Ngido alieleza kwamba, pamoja na ujenzi wa barabara hiyo , tayari kampuni ya Barrick imetumia zaidi ya shilingi bilioni mbili katika ujenzi wa miundombinu ya barabara ikiwemo mitaro ya maji katika kijiji cha Kakola na Bushingwe na ujenzi wa Chuo cha Ufundi cha VETA cha Bunango, miradi ya afya na elimu katika vijiji vinavyozunguka mgodi Bulyanhulu
Naye , Mwenyekiti wa kijiji cha Ilogi Edward Shija alisema kuwa utekelezaji wa mradi huo umeanza vizuri kwa kuwashirikisha wananchi kuanzia hatua za awali ambapo kukamilika kwa barabara hiyo kutawezesha wananchi kufika kwa haraka katika maeneo mengine yanayoungana na wilaya ya Kahama na vitongoji vyake ili kupata huduma mbalimbali ikiwemo Biashara , Afya na Elimu.
CHANGAMOTO ZA WATUMISHI WA UMMA ZITATULIWE ILI KUKUZA SEKTA YA UMMA KIUCHUMI NA KIJAMII
Na. Veronica Mwafisi-Arusha
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amewaasa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) kuwa wabunifu katika kusimamia vizuri rasilimaliwatu ili kuondokana na changamoto mbalimbali za watumishi wa umma na kukuza sekta hiyo kiuchumi na kijamii ili kuleta maendeleo makubwa katika Bara la Afrika.
Mhe. Simbachawene ametoa kauli hiyo alipokuwa akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa kufungua Mkutano wa 9 wa Mtandao wa Mameneja wa Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
“Mkutano huu wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu umefanyika katika kipindi ambacho dunia ina changamoto mbalimbali hivyo niwaase mtumie fursa ya mijadala mtakayoiendesha na mawazo mtakayoyatoa kupitia maazimio na mapendekezo yalete mtazamo chanya katika kutoa majawabu yatakayosaidia kukuza sekta ya umma kiuchumi na kijamii.” Amesema Mhe. Simbachawene
Mhe. Simbachawene ameongeza kuwa, kupitia kaulimbiu ya mkutano huo inaonyesha ni kwa namna gani rasilimaliwatu katika utumishi wa umma ni nyenzo muhimu na ya thamani kubwa katika kila nchi ambapo Serikali huitumia kuwafikia wananchi wake katika kutoa huduma za kijamii na kiuchumi ili kukuza ustawi wa jamii husika.
Aidha, Mhe. Simbachawene amewapongeza wawezeshaji wa Mkutano huo kwa mada mbalimbali walizozitoa kabla ya kufunguliwa kwa mkutano huo ambazo kwa asilimia kubwa zitasaidia kuleta mabadiliko katika utendaji kazi kupitia rasilimaliwatu zilizopo katika Bara la Afrika.
Kwa upande wake, Rais wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi, amesema kuwa katika mkutano huo wa 9 wajumbe watapata fursa ya kubadilishana uzoefu na utaalamu kwa lengo la kuwezesha nchi za Bara la Afrika kupiga hatua za kimaendeleo kwa kutumia mbinu za kisasa.
“Mtandao huu umeanzishwa kwa lengo la kujenga uwezo wa rasilimaliwatu yenye matokeo chanya katika kuhudumia wananchi Barani Afrika hivyo kupitia Mkutano huu tutapata fursa ya kubadilishana uzoefu na utaalamu ili kuzisaidia nchi zetu kujikwamua kiuchumi na kuleta maendeleo kwa mataifa.” Bw. Daudi amesema.
Mkutano huo wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMNet) uliofunguliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan unatarajiwa kufanyika kwa muda wa siku nne kuanzia leo tarehe 4 hadi 7 Novemba, 2024 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC) jijini Arusha.Kaulimbiu ya Mkutano huo ni ‘Utawala Stahimilivu na Ubunifu: Kukuza Sekta ya Umma ijayo kupitia Uongozi wa Rasilimaliwatu’.
TANZANIA NA UGANDA ZAKUTANA KUJADILI UIMARISHAJI MPAKA WA KIMATAIFA
Kikao cha Kamati ya Pamoja cha Wataalamu wa Tanzania na Uganda (JTC) kimeanza mkoani Kagera nchini Tanzania kujadili uimarishaji mpaka wa kimataifa baina ya nchi hizo.
Kikao hicho kimeanza tarehe 5 Novemba 2024 na kutarajiwa kumalizika Novemba 7, 2024 kinafanyika katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera na kuhusisha wataalamu kutoka nchi za Tanzania na Uganda.
Akifungua kikao hicho cha siku tatu kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Abuubakar Mwasa, katibu Tawala mkoa wa Kagera Bw. Stephen Ndaki amesema, Tanzania imejipanga kikamilifu kutekeleza zoezi la uimarishaji mpaka wa kimataifa kwa ajili ya ustawi wa nchi hizo mbili.
Amebainisha kuwa, uimarishaji mpaka wa kimataifa kati ya Tanzania na Uganda una lengo la kuweka usimamizi mzuri wa mpaka baina ya nchi hizo pamoja na kukuza amani, upendo, usalama na maisha ya watu wake.
Kupitia hotuba hiyo ya Mkuu wa mkoa wa Kagera, Bw. Ndaki amesema, Tanzania na Uganda zimekuwa na mahusiano mazuri ikiwemo tamaduni zinazofanana alizozieleza kuwa, zimewezesha wananchi wa nchi hizo mbili kuishi kwa upendo.
"Ni imani yangu kila mshiriki katika kikao hiki atatumia muda kuhakikisha uimarishaji mpaka wa kimataifa baina ya nchi zetu unakuwa na matokeo mazuri kwa ustawi wa nchi na wananchi wetu" amesema.
Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni mkuu wa timu ya Tanzania katika kikao hicho Bw. Hamdouny Mansoor amesema, mkutano huo ni utekelezaji wa mpango wa Umoja wa Afrika kuhusu uimarishaji wa mipaka ya kimataifa kwa nchi za Afrika kufikia mwaka 2027.
"Ni nia ya Umoja wa Afrika kuzifanya nchi za Afrika kuwa na amani pasipo migongano wakati wa zoezi zima za uimarishaji mipaka ya kimataifa" amesema Mansoor.
Kwa upande wake Mkuu wa ujumbe wa timu ya wataalamu kutoka Uganda Bi. Jacqueline Banana Wabyona ameihakikishia Tanzania ushiriki mzuri kwenye kikao hicho kwa lengo la kufikia matokeo chanya ya uimarishaji mpaka kati ya Tanzania na Uganda.
Mpaka wa Tanzania na Uganda una urefu wa takriban km 397.8 ambapo kati ya hizo km109 ni nchi kavu , km 42.8 ni sehemu ya mto kagera na km 246 ni sehemu ya ziwa victoria.
Zoezi la uimarishaji mipaka ya kimataifa ni utekelezaji wa makubaliano ya Umoja wa Afrika kuwa, ifikapo mwaka 2027 mipaka baina ya nchi za Afrika iwe imeimarishwa.
Tanzania imepakana na nchi 10 ambazo ni Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, DRC, Zambia, Malawi, Msumbiji, Comoro na Shelisheli huku mipaka baina ya nchi hizo ikiwa imegawanyika katika sehemu mbili za nchi kavu na majini.
WAZIRI KOMBO AFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA CUBA
Mazungumzo ya viongozi hao yalijikita katika kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimaendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo,sekta ya afya, teknolojia, dawa na vifaa tiba, masuala ya uhamiaji, Utalii, uwekezaji, biashara, utamaduni Sanaa na michezo na elimu.
Vilevile, ameeleza kuwa Tanzania itaendelea kuimarisha ushirikiano wake na Cuba ikiwa ni pamoja na kuunga mkono jitihada zake za kupinga vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Cuba ili kwa pamoja nchi hizo ziweze kutekeleza kwa tija program za ushirikiano wa kimaendeleo.
Naye Mhe. Parrilla ameishukuru Tanzania kwa kuendelea kuiunga mkono Cuba katika mapambano ya kupinga vikwazo vilivyowekwa na Marekani. Pia aliongeza kuwa Cuba imefurahishwa na msimamo wa Tanzania uliotolewa hivi karibuni kupitia hotuba ya Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa ambapo Tanzania iliunga mkono azimio lingine la Umoja wa Mataifa la kupinga vikwazo vya Marekani dhidi ya Cuba
‘’Tunamsubiri Rais Samia awasili nchini Cuba kwakuwa maandalizi yameshakamilika na kupitia ziara hii tuna imani kwamba ushirikiano wetu utazidi kuimarika. Pia fursa zitakazoletwa na kongamano la kimataifa la Kiswahili litaifanya Cuba kuwa kitovu cha lugha ya Kiswahili katika ukanda wa Caribbean na sasa vyuo vikuu vya Cuba vimeanza kufundisha lugha ya Kiswahili kama moja ya somo la lugha ya kigeni.’’ alieleza Mhe. Parrilla.Tanzania na Cuba ni washirika wa muda mrefu, tangu enzi la ukombozi wa bara la Afrika ambapo ushirikiano huo umeziwezesha nchi hizo kuendelea kuthamini na kusimama pamoja katika masuala mbalimbali yaliyopelekea kuichagua Cuba kuwa mwenyeji wa kongamano la Kiswahili litakaloenda sambamba na uzinduzi wa kamusi ya kispanyola - kiswahili wakati wa Ziara ya Kitaifa ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.Viongozi wengine walioambatana na Mhe. Waziri Kombo ni pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Muungano waTanzania nchini Cuba, Mhe. Humphrey Polepole, Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi Naomi Mpemba na maafisa waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Cuba.