Saturday, February 6, 2010

JK na mkwara wa flyovers!

Mkuu wa nchi Rais JK,amechimba biti kwa wahusika kuwa sasa umefika wakati wa kuwa na barabara zinazopita juu kwa juu (flyovers) kupunguza misongamano ya magari katika Jiji la Dar es Salaam.

Akichimba biti hilo ndani ya ukumbi wa Karimjee ..huku tukiwa kwenye safari ya kuelekea uchaguzi mkuu...JK alisema ''Hili la flyovers lipewe kipaumbele ili tupunguze msongamano wa magari katika Dar es Salaam...tusipofanya hili jiji hili litakuwa halipitiki katika muda wa miaka mitano, ama hata katika miaka miwili ama mitatu ijayo,''

Rais Kikwete pia ameagiza wataalamu wa mipangomiji kuanza kupunguza maeneo yasiyopimwa katika jiji hilo kwa kuwa ni asilimia 30 ya Jiji la Dar es Salaam ambako watu wamejenga katika maeneo yaliyopimwa.

Amesema, Jiji la Dar es Salaam haliwezi kuendelea kupanuka bila kupangiliwa.

''Hatuwezi kuendelea namna hii na mji unaopanuka namna hii. Hili ni jambo zito, kubwa linalohitaji umakini wa haraka kutatuliwa. Ndio maana kipindupindu hakiishi katika mji huu.'' Amesema.

No comments: