Timu ya Taifa ya Ivory Coast.
Na Erasto StanslausIVORY Coast na Cameroon ni kati ya timu zilizoalikwa katika michuano ya Kombe la Challenge, itakayofanyika kuanzia Novemba 27 hadi Desemba 11, mwaka huu itajayofanyika jijini Dar es Salaam.
Michuano hiyo inayofanyika kila mwaka, inashirikisha nchi za Afrika Mashariki na Kati ikiwa chini ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), ambapo mwaka huu itakuwa na timu zaidi ya 12.
Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicolaus Musonye, aliliambia Champion Ijumaa kuwa, Ivory Coast ambao tayari wamethibitisha kushiriki michuano hiyo huku Cameroon wakiahidi kuthibitisha wiki ijayo, lakini pia Zambia na Malawi zimeomba kushiriki.
“Michuano ya mwaka huu itakuwa bora kutokana na udhamini mkubwa kutoka kwa kampuni ya Serengeti Breweries wa zaidi ya Sh. milioni 675, zitakazogharamia michuano yote ikiwa pamoja na timu zitakazoshiriki,” alisema Musonye ambaye aliiombea Taifa Stars iifunge Morocco kesho katika mchezo wa awali wa Kombe la Mataifa ya Afrika.
Musonye alizitaja timu zitakazoshiriki michuano hiyo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Djibouti, Somalia, Ethiopia, Tanzania, Zanzibar na Eritrea, ambazo zitaungana na Ivory Coast, Cameroon na Zambia na Mawali kama wakikubaliwa.
HABARI KWA HISANI YA GPL
No comments:
Post a Comment