ANGALIA LIVE NEWS

Friday, October 8, 2010

Ndugu Wapendwa - Tumsifu Yesu Kristu !

 Ni matumaini na sala yangu ya kuwa nyote mnaendelea vizuri.
Baada ya ile Misa yetu ya Kiswahili - Septemba 5. Tulipokea maombi mbali mbali kwa njia ya simu na email mkiomba ibada nyingine ya Kiswahili ifanyike tena, Baada ya hapo Kikao cha watu wachache kilikutana Septemba 19, kutathmini ibada iliyopita na kuona kama kuna umuhimu wa kufanya tena misa nyingine. Taarifa ya hiyo kikao ilitumwa kwenu na Baraka Daudi (Katibu wa Kikao). Asante Baraka. 
      Kikao kiliamua tuwe na misa mbili mpaka mwaka mpya. Novemba 7 na Desemba 26.
     Mimi pamoja na Pd. Evod Shao na wanakamati tunafurahi kutangaza ya kuwa Misa nyingine Takatifu kwa lugha ya Kiswahili itakuwa NOVEMBA 7SAA NANE (8:00) MCHANA, pale St.Camillus kwenye jengo la GYM. Anuani ya St.Camillus iko hapo chini.
     Katika kuifanikisha hilo tukio kuna watu watakao ratibu; Litrujia; nyimbo,masomo, mapaji,watumishi; Chakula na Vipaji. Wakiomba ushirikiano wako uwe mkarimu ili tuweze kuifanikisha tukio hili tena kwa umoja,furaha na upendo.
      Ingawa Misa inaratibiwa na Watanzania na itakuwa kwa lugha ya Kiswahili kwa sheria ya Kanisa Katoliki la Roma. Kwenye misa anakaribishwa mtu yeyote; Mtanzania na asiye Mtanzania, anayezumgumza Kiswahili na asiye zungumza; Mkatoliki/Mkristu na asiye.
      Niwatakie yote mema na Tuzidi Kuombeana

     Katika Kanisa na Utumishi

      Fr.Wolfgang Pisa,ofmcap




St Camillus Parish 
1600 St Camillus Dr 
Silver Spring, MD 20903


No comments: