ANGALIA LIVE NEWS

Monday, October 4, 2010

NI AJABU LAKINI NI KWELI???KAMA UNABISHA NENDA MAENEO YA MBURAHATI KWA JONGO ULIZIA....

Juzi jumanne nilipokea ujumbe kwenye simu yangu ya mkononi iliyosomeka KUNA TUKIO LA AINA YAKE,KUNA MDADA ANAWAKA MOTO BILA SABABU lakini maumivu hasikii tena kila anapokuwa unawaka hata akija kwako kukutembelea moto huwaka..Huku mburahati kwa jongo.

Kiukweli meseji hii ilinishangaza ikabidi nimwambie mama wa hekaheka Gea Habib aende akafatilie kunani?

Kufika huko ni kweli kabisa maana tukio hilo linamshangaza kila mtu hata wewe ukiweza nenda ulizia utapelekwa mpaka nyumbani kwa huyo dada.
Dada mwenyewe ndio huyu anaeonekana kidogo kwenye picha maana hakutaka kupigwa picha.Ni mjamzito hapo alipo ila hali ndio hiyo akiwa mahali hata kama ni kwako akikaa peke yake moto unawaka aidha kwenye nguo zake,kochi,kitanda,hata kama ni nguo iliyotundikwa inawaka moto.Mpaka sasa haijaeleweka ni kwa nini mashekhe wamemuombea dua toka juzi hiyohiyo ambapo alilala msikitini.

Wapo waliosema labda kachukua mume wa mtu kafanyiwa mchezo lakini alipoulizwa akasema huyo mwanaume mwenye mimba wamefunga ndoa na anavyojua kamkuta hana mwanamke labda awe kamdanganya.
Dada wa watu hana raha kabisa ndugu zake inabidi wakae nae kama kumetokea msiba maana ni kitu cha ajabu sana kilichompata ndugu yao maana kimeanza wiki hii hapa.


Nguo mbalimbali zilizo ungua kwa nyakati tofauti....




Hili godoro liliungua wakati yeye amelala kitandani,likashika moto






Nguo zilizoungua na zinaungua akiwepo yeye eneo hilo



Vitenge,nguo alizopewa na ndugu kuvaa pia ziliwaka kwa nyakati tofauti kwa siku unaweza kuwaka hata mara sita

Alikuwa amekaa kwenye kochi kochi likaanza kuwaka moto,na lazima moto ukiwaka awe peke yake akija mtu mwingine unazima unabaki moshi. 

Hapo nyumbani inabidi ndugu wakae na ndugu yao maana moto huo unawaka akiwa peke yake bila watu,kukiwa na watu hauwaki.
Ndugu wengi wamekusanyika hapo nyumbani kama kuna msiba vile,ili kukaa na ndugu yao kumfariji na kuhakikisha anakuwa sawa. 
Ndugu wakiwa katika hali ya simanzi kama kuna msiba kwa hicho kilichomkuta ndugu yao.

Kaka wa mhanga wa tukio hilo akionyesha godoro lingine lililoungua kimaajabu.
Mwisho kabisa moto huu haumuunguzi,wala hasikii maumivu ya aina yoyote zaidi ya hofu na wasiwasi wa kutokujua nini kipo nyuma ya huu moto.


Habari na picha kwa hisani ya Dina Marios

No comments: