Mustakabali wa soka ya Ghana unakabiliwa na giza baada ya maafisa wa kitengo cha kupambana na rushwa, kuzingira makao makuu ya chama cha soka cha nchi hiyo (GFA) siku ya Jumanne.
Maafisa wa Kitengo cha kupambana na rushwa wa Ghana, wamewazuia maafisa wa chama hicho kuingia au kutoka katika ofisi za chama hicho mjini Accra, wakiwa wanatafuta nyaraka ambazo hazijafahamika.
Maafisa hao wamesema, wamepata kibali cha upekuzi kutoka mahakamani, wamechukua kompyuta na simu za mikononi kutoka ndani ya jengo hilo.
Kwa kawaida shirikisho la soka duniani- Fifa linakuwa na msimamo mkali kutokana na serikali kuingilia mambo ya uendeshaji wa vyama vya soka vya nchi.
Kutokana na hulka hiyo ya serikali, nchi nyingi zimekwishafungiwa na Fifa kujihusisha na masuala ya soka siku zilizopita.
Rais wa GFA, Kwesi Nyantakyi, hakuwepo ndani ya jengo la makao makuu ya ofisi za chama cha soka, lakini alitarajiwa kuwasili wakati wowote.
Hatua hiyo imekuja wiki moja baada ya Fifa kuionya serikali ya Ghana juu ya uwezekano wa kuwekewa vikwazo iwapo itaingilia uendeshaji wa soka ya nchi hiyo.
Ikiwa imechunguza madai ya kuingilia shughuli za soka, Fifa iligundua soka ya Ghana inachagizwa na serikali kuhusiana na masuala yaliyojitokeza hivi punde.
Mfano mmoja ilikuwa ni jaribio la serikali ya Ghana, kutaka kumuweka madarakani Abedi Pele kuwa mgombea kwa nafasi iliyowazi ya mjumbe katika Shirikisho la soka barani Afrika licha ya GFA kupinga wazo hilo
No comments:
Post a Comment