ANGALIA LIVE NEWS

Monday, December 6, 2010

Mbeki aenda Ivory Coast

Rais wa zamani wa Afrika Kusini amewasili nchini Ivory Coast kuwakilisha Umoja wa Afrika kusaidia kusuluhisha mzozo wa kisiasa.
Mbeki
Thabo Mbeki
Laurent Gbagbo na mgombea wa upinzani Alassane Ouattara wote wamekula kiapo cha kuongza nchi, baada ya kudai kupata ushindi katika raundi ya pili ya uchaguzi.

Awali Bw Ouattara alitangazwa mshindi, lakini matokeo hao yalitenguliwa na kupewa Bw Gbagbo anayetetea kiti chake.
Umoja wa Afrika umeonya kuwa mzozo huo unaweza kuleta "matatizo makubwa".
Katika taarifa iliyotolewa, umoja huo umezitaka "pande hizo mbili kuonesha uvumilivu na kujizuia kuchukua hatua ambazo zitaleta matatizo katika hali ambayo ni tete".
Nchi kadhaa na mashirika ya kimataifa - ikiwemo marekani, Umoja wa Mataifa Ufaransa na Shirika la Fedha Duniani IMF - zimeunga mkono kutangazwa kwa Bw Ouattara kuwa mshindi wa kura hiyo iliyopigwa Jumapili iliyopita.
Bw Mbeki aliwasili mjini Abidjan Jumapili asubuhi, ikiwa ni mara ya kwanza kufunguliwa kwa mipaka ya nchi hiyo, tangu ilipofungwa siku ya Alhamisi wakati mzozo huo ulipoibuka.
Wakati akiwa rais wa Afrika Kusini, Bw Mbeki alisaidia kufikia makubaliano ya amani nchini Ivory Coast.
Wasiwasi ni kuwa, iwapo atashindwa kufikia suluhu yeyote, makundi ya waasi ya upande wa kaskazini ambayo yanamuunga mkono Bw Ouattara, yatabeba silaha kupinga hali ilivyo.
Bw Ouattara alitangazwa mshindi siku ya Alhamisi na Tume Huru ya Uchaguzi ya Ivory Coast, lakini siku ya Ijumaa matokeo hayo yalipinduliwa na Baraza la Katiba, ambalo linaongozwa na mshirika wa Bw Gbagbo.

No comments: