ANGALIA LIVE NEWS

Friday, December 3, 2010

UHUSIANO KATI YA SWAHILI NA MOZAMBIQUE FASHION WEEK WAIMARIKA MANJU MSITA KUIWAKILISHA SWAHILI FASHION WEEK SWAHILI FASHION WEEK KUSHEREKEA SIKU YA UKWIMWI DUNIANI VISIWANI ZANZIBAR

Kutoka kushoto ni Hamis Omary, Manju Msita and Saphia Ngalapi, PR & Media Manager Swahili Fashion Week, During the press conference at Habari Maelezo, Dar es Salaam
Kutoka kushoto ni Hamis Omary, Marketing Manager Swahili Fashion Week and Maju Msita Designer, speaking with journalist during the press conference. at Habari Maelezo
Manju Msita - designs
Manju Msita - designs
Ni awamu ya sita kwa tamasha kubwa la kila mwaka Mozambique fashion week litakalofanyika kuanzia tarehe 6-11 Disemba mjini Maputo Msumbiji. Mahusiano kati ya Swahili na Mozambique fashion week yalianza mwaka 2009 kwa washiriki Adelia na Sheila Tique kuiwakilisha Msumbiji katika Swahili fashion week 2009 na baadaye Swahili fashion week iliwakilishwa na Jamira Vera Swai.


“Mwaka huu Marinella Rodriguez aliiwakilisha Mozambique Fashion Week katika  Swahili fashion week, kwa heshima na furaha  kubwa tunajivunia kumchagua Manju Msitta kuiwakilisha Swahili fashion week katika tukio muhimu mjini Maputo siku ya tarehe 11 Disemba” alisema Mustafa Hassanali muanzilishi wa Swahili Fashion Week.

“Ni furaha kubwa kuiwakilisha Tanzania na Swahili fashion week katika maonesho ya Mozambique Fashion Week mwaka huu. Nina imani nitaipeperusha vizuri bendera ya Tanzania na Afrika mashariki katika tukio hili la kidunia.” Alisema Manju msita

Manju alichaguliwa na muandaaji wa maonesho ya mavazi wa kimataifa Jan Malan Umzingeli kwa kushirikiana na Swahili Fashion Week kwa kigezo kwamba kazi zake zina kiwango cha juu kulingana na ubora wa ubunifu wa mavazi yake.

“Huu ni mwanzo wa kuimarisha mahusiano baina yetu, na sio siasa pekee inayotuunganisha Tanzania na Msumbiji ila kupitia Utamaduni pia unatuunganisha.Uhusiano huu uendelee zaidi na kuwa imara mwaka hadi mwaka.” aliongeza Hassanali.

Kwa upande mwingine Swahili fashion week itaandaa sherehe ya SIKU YA UKIMWI DUNIANI siku ya tarehe 4 Disemba katika ukumbi wa Mercury’s Zanzibar, tukio hilo limeandaliwa kwa kushirikiana na Explore Zanzibar kwa lengo la kutunisha mfuko wa ZAPHA+ (Zanzibar Association of People Living with HIV/AIDS) msherehehaji katika sherehe hiyo atakua Abby Platjees na mziki utaporomoshwa kutoka kwake DJ Eddy kutoka Zanzibar, itakua ni kusherehekea usiku mzima.  

“Ni jukumu letu na kwa kila mmoja wetu na jumuiya kuleta maendeleo ya kiuchumi na jamii huku tukijua ya kwamba Swahili Fashion Week imelenga katika kuwasaidia watu waishio na virusi vya ukimwi. Kati ya jumuiya hizo Tanzania Mitindo House imekua ikipewa misaada kwa miaka 3 sasa na ni matumaini yetu kuwa tunaweza kuendelea na kufika mbele zaidi ndani ya Tanzania” alikamilisha Hassanali

KWA WAHARIRI

KUHUSU SWAHILI FASHION WEEK
Swahili fashion week ni jukwaa la wabunifu wote katika mavazi na vito kutoka katika nchi zinazozungumza lugha ya Kiswahili na kuonesha ubunifu wao, kutangaza sanaa zao ili kupata wateja wa bidhaa zao. Hii yote imelenga katika kukuza sanaa ya maonyesho ya mavazi na kujipatia kipato, kutengeneza ajira ili kuhamasisha katika lengo la kuwa na (Bidhaa kutoka Afrika Mashariki)

Swahili fashion week imekua ya kila mwaka ili kuonesha uzuri zaidi na vipaji katika ubunifu kwa nchi zinazozungumza lugha ya Kiswahili. Hii imefanya kuwa tamasha kubwa la fashion katika afrika mashariki lililobuniwa na kufanikishwa mwaka 2008 na mbunifu mkubwa Mustafa Hassanali.
                                                                       
“Ili kuanzisha kitu cha tofauti na chenye kuleta matumani katika ubunifu wa jukwaa la maonesho ya mavazi, Swahili fashion week imekua moja ya tamasha kubwa la maonesho ya mavazi kwa ukanda wa Afrika Mashariki na katika soko la kimataifa”alieleza Mustafa Hassanali, muanzilishi na muandaaji wa Swahili Fashion Week.

KUHUSU MANJU MSITA
Manju Msita ni mmoja kati ya wabunifu wenye ubunifu wa hali ya juu nchini Tanzania akiwa kama graphic designer, aliingia katika muziki na hatimaye katika sanaa ya mavazi. Manju anapinga kiuga sanaa za wengine, anajichukulia kama mbunifu wa pekee. Nabuni mitindo tofauti kutoka kwangu hadi kwa wateja wangu

Manju amekua hana mpinzani katika ubunifu wa mavazi ya kiafrika na imemfanya akubalike na kuwa wa kwanza katika tasinia hii na imara zaidi, kupitia kampuni yake ya Smart Africa, iliyopo katika jingo la Mikono Art Complex karibu na VETA, Dar es salaam. Manju ameanzisha mavazi katika ladha ya kiafrika, kitchen party, send-off, harusi, ofisi, dhifa tofauti ikiwemo viatu,hii imekua ni zaidi ya fashion, mavazi hayo yakiwa katika rangi za kuvutia na tofauti, kwa manju huu ni ulimwengu mpya kwake.pamoja na ubunifu wake sasa manju ameng’ara kila kona, manju ambaye alizindua na kuanza ubunifu wa mitindo katika miaka ya 1990, hayo ni mafanikio aliyoyapata ndani ya ulimwengu wa sanaa na mitindo, haikua bure ila mwanzo mzuri wenye mafanikio.

KUHUSU MOZAMBIQUE FASHION WEEK
Mozambique Fashion Week (MFW), ni tamasha la sanaa na utamaduni na ni pekee nchini Msumbiji linalounganisha wabunifu na linalovumbua vipaji mbalimbali ikiwemo ubunifu wa mavazi, pia limelenga kuleta ajira na kufungua njia mipya ya bishara na masoko na mawasiliano ya wataalamu katika suala zima la mitindo nchini Msumbiji na kimataifa.

Mozambique Fashion Week ina malengo ya kuimarisha mitindo kitaifa na pia kupanua wigo wa soko la mitindo nchini humo, ikiwemo kuibua vipaji vipya nchini kote.
MFW imeleta chachu ya maendeleo ya mitindo ya Mozambique fashion na kuwa kivutio kikubwa cha utalii nhini na kutangaza utamaduni wan chi ya msumbiji na kukuza ubunifu wa mitindo kimataifa.

 Saphia Ngalapi
Media & PR Manager
Mustafa Hassanali
PO Box 10684, Dar es Salaam, Tanzania
105 Kilimani Road,   Kinondoni, Dar es Salaam, Tanzania
(opp. Patricia Metzger Health & Beauty Clinic / near French Embassy)
Tel :  +255 (0)22 266 8555
Mobile :  +255 (0)712 099 834
Mail : media@mustafahassanali.net
Web : www.mustafahassanali.net
www.swahilifashionweek.com
www.harusitradefair.com
www.twende.info

No comments: