ANGALIA LIVE NEWS

Friday, January 28, 2011

Waliopoteza maisha Zanzibar maandamano ya 2011 wakumbukwa

Na Salma Said,
CHAMA Cha Wanachi (CUF) jana kimeadhimisha miaka 10 ya maombolezo ya vifo vya wananchi vilivyotokea Januari 26-27 mwaka 2001 katika maandamano ya amani yaliyofanyika Zanzibar huku kikiwa na ujumbe wa kutaka suala kama hilo la aibu lisitokee tena nchini.
Mkurugenzi wa habari uenezi mawasiliano ya umma na Haki za binadamu wa chama hicho, Salim Bimani alisema Tanzania kwa mara ya kwanza ilipata aibu kubwa ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu uliofanywa na vikosi vya ulinzi na usalama jambo ambalo linapaswa kuepushwa na lisitokee tena kwa kuwa kitendo hicho kimeitia doa Tanzania katika sura za kimataifa.
“Tunaadhimisha siku ya wauaji Zanzibar kimya kimya tofauti na siku za nyuma tulikuwa tukifanya mkutano wa hadhara na kuwakusanya waathirika wote lakini sasa tunasema tutasoma khitma kila wilaya na mkoa na kuwaombea wenzetu wlaiotangulia mbele ya haki katika tukio lile” alisisitiza Bimani.


Alisema hayo yaliotokea ambayo ni sawa na mauaji yake yaliofnayika Arusha mwanzoni mwa mwezi huu ni kutokana na katiba mbaya zilizopo nchini kwani bado demokrasia inahitaji kupewa nafasi yake hasa kwa kuwa Tanzania iliridhia mfumo wa vyama vingi.
Akitoa kasoro za kikatiba Bimani alisema kufnaya maandamano ni haki ya msingi ya kikatiba lakini jambo la kushangaza jeshi la polisi huwa linatafuta sababu nyingi kuwadhibiti wananchi wasiandamane licha ya kuwa hiyo ni moja ya haki yao ya msingi.
Akikazia kauli yake Bimani alisema wakati umefika wa kuandikwa katiba mpya na sio viraka kwa serikali zote mbili ya Muungano na ile ya Zanzibar kwani kufanya hivyo itakuwa ni sehemu ya kuwaunga mkono wanaharakati wote waliopoteza roho zao katika maandamano hayo.
“Hapa jambo la msingi kabisa na zuri kabisa ni kuandikwa kwa katiba mpya itakayowahsirikisha wananchi wote wa nchi hizi ….katiba itakayokidhi matakwa ya wananchi …katiba ambayo itakuwa inaendena na wakati husika maana katiba tulionayo ni ile ya mfumo wa chama kimoja tukumbuke kwamba sasa tuna mfumo wa vyama vingi lakini pia tunahitaji katiba ambayo itakuwa inakwenda sambamba na uhuru a kutoa fursa ya demokrasia ya kweli kwa umma” alisema Bimani.
Alisema kudai katiba mpya ni haki ya umma wa Tanzania ambao wanapaswa kutoa maoni katika kuiletea maendeleo nchi yao lakini pia ni kuiepusha nchi na kasoro kama hizo za majanga na malalamiko ya wanaanchi dhidi ya serikali yao.
Akirudia katika tukio la mauaji ya raia wasio na hatia alisema chama chake kitaendelea kuwakumbuka wahanga hao kwnai ndio walioleta ukombozi na kwamba kitendo kama hicho kikiwa kinakumbukwa ndipo viongozi watakapoweza kukumbuka maovu yao waliotenda dhidi ya wananchi wao wasio na hatia lakini pia vizazi vitaweza kujua kilichotokea kwa wazee wao.
Alisema kuna kila sababu ya siklu hiyo kuadhimishwa kwa kuwakumbuka wahanga kwani walipoteza roho zao walikuwa wakidai haki yao ya msingi ya kuandamana na kutaka demokrasia ichukue mkondo wake chini ya mfumo wa vyama vingi.
Bimani alisema mauaji ya Unguja na Pemba na yale yaliotokea Arusha hivi karibuni iwe ni funzo na onyo kwa serikali na jamii pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kutorejea tena katika janga hilo la umwagikaji damu na kujisahihisha ili siku za baadae lisije likatokea tena na kuiingiza nchi katika matatizo na kuondoshwa jina zuri la Tanzania ni nchi ya amani.
Alisema vifo vilivyotokea havitasahaulika kwa kuwa vimeacha alama kubwa nchini ikiwmeo vizuka, vilema ambao wamepoteza viungo vyao kutokana na maandamano hayo pamoja na kubakiza kumbukumbu kuwa ya mayatima kadhaa hivyo alisema suala hilo linahitaji kufikiriwa na serikali kujipanga upya ya kujua namna gani ya kuweza kukabiliana na wananchi bila ya madhara hasa kwa kuiga nchi za jirani ambazo hufanikiwa kutoa uhuru wa kuandamana bila ya jeshi la polisi kuingilia kati na kupiga au kuuwa.
Kiongozi huyo alisema kawaida huwa wanaadhimisha siku hiyo kwa kufnaya mkutano w ahadhara na maandamano lakini mara hii amewataka kufnaya maombolezi ya kimya kimya katika maeneo yao kwa kuendesha sala na dua maalumu za kuwaombea wahanga na waliofikwa na maafa hayo.
Hivyo amewataka wale wote waliopatwa na maafa juu ya tukio hilo la huzuni kujumuika pamoja katika maombolezi hayo ambapo kusoma dua na sala katika wilaya zote kuwaombea muhanga hao waliopoteza maisha yao siku kama hiyo.
Aidha Mkurugenzi huyo aliomba serikali ya Muungano kama ilivyopendekezwa na ripoti iliyoundwa na rais mstaafu wa Jamhuri ya Tanzania William Benjamin Mkapa , Tume ya Hashim vita juu ya mapendekezo ambayo yaliwasilishwa serikalini ya kuweza kufidia wale waliopatwa na maafa na kudhurika kwa namna moja au nyengine katika hadhia hiyo.
Aliomba serikali ya Jamhuri ya Muungano suala hili walimalize ili liweze kutekelezwa kama vile mapedekezo hayo yalivyotoka na vilevile alibainisha ya kwamba suala hili ni jambo la kufa basi litaendelea kukumbukwa kila ifikapo siku hiyo ya januari 26 na 27.
Pia ameiomba serikali kutekeleza juu ya yale madai ambayo waathirika waliyodai juu ya kufanywa kwa marekebisho ya katiba mpya katiba zitazokuwa za kidemokrasia zitakazoungwa mkono na umma.
Aidha alisema hilo itakuwa ni sehemu ya kuwaunga mkono wanaharakati hao waliopoteza maisha yao na wengine waliopoteza kwa namna mbali mbali katika njia ya kupigania uhuru katika ukombozi wa kileo na kifikra na wakimabadiliko itakuwa na wao imewashirikisha kwa kupata katiba mpya .
Alisema hilo ndio lengo la watanzania wote kuiendesha nchi yetu na kuiepusha isije ikarudia tena katika majanga kama yale au mengine kuliko hayo na kuweka mustakabali mpya wa salama usalimini wakuwaweka watanzania katika umoja amani na mashirikiano.
Januari 26 na 27 zaidi ya watu 40 walipoteza maisha kutokana na kufuatuliwa risasi n ajeshi la polisi kwa madai ya kuandamana bila ya kibali cha jeshi hilo ambapo mamia ya wazanzibari walikimbilia Mombasa Kenya na Somalia ikiwa ni mara ya kwanza Tanzania kutoa wakimbizi kutoka Zanzibar

No comments: