Ndugu Zangu,
KIONGOZI wa nchi haui watu wake, Moummar Gaddafi amewaua. Ndio, mchana wa jua kali, na bado anasimama, anadai ni kiongozi wa WaLibya, Gaddafi hana aibu.Anapostahili kusimama Gaddafi sasa si kwenye jengo la Ikulu ya Tripoli, bali Mahakama ya Kimataifa Ya Haki na inayoshughulika na Wahalifu wa Kivita, The Haag.
Baraza la Usalama la Umoja Wa Mataifa jana limepitisha azimio la kumwekea Gaddafi vikwazo vya silaha na kugandisha amali zake. Inasemekana, Gaddafi ana akaunti za mabilioni ya dola za KiMarekani. Kumwekea Gaddafi na familia yake vikwazo ni msaada mkubwa kwa watu wa Libya kwa sasa.

Kosa kubwa kabisa alilofanya Gaddafi kwa WaLibya ni KUWAKANDAMIZA. Ndio, kuwanyima UHURU. Gaddafi aliwafanya WaLibya kama ng’ombe kwenye zizi. Waliotoa sauti kumpinga aliwakamata na ‘kuwachinja’, kimyakimya.
Libya ikawa mali ya Gaddafi na familia yake. Wanaodai haki yao sasa anaowaona kuwa ni majambazi wanaovamia nyumba yake. Kumbe! Jambazi mkubwa kwa WaLibya alikuwa ni Gaddafi na familia yake. WaLibya, kama wenzao wa Tunisia na Misri, wameamka. Hawatalala tena mpaka Gaddafi na familia yake wameondoka madarakani.
Naam. Gaddafi bado anang’ang’ania madarakani. Ameshindwa kusoma alama za nyakati, kabla na sasa. Ninavyofuatilia yanayoendelea Libya na ulimwengu mzima wa WaArabu, naziona kila dalili, za Gaddafi kutomaliza hata wiki moja kutoka sasa akiwa madarakani.
Gaddafi anatumia kila mwanya na hila, kujaribu kuurudisha nyuma mshale wa saa ya mabadiliko. Huko ni sawa na kulizuia wimbi la bahari kwa mikono. Hakika, WaLibya hawastahili tena kuongozwa na mtu kama Gaddafi. Ni Gaddafi huyu wa sasa, amewadhalilisha watu wake mbele ya macho ya walimwengu, anaendelea kufanya hivyo.
Si tumeona Ijumaa jioni , amesimama na kuwaambia WaLibya waendelee kuimba na kucheza! Gaddafi amepoteza mwelekeo na mguso wa hali halisi. Amepitisha viwango vyote vya ulevi wa madaraka, Gaddafi wa sasa anaonekana kama mwehu fulani aliyeshika bunduki na kupita mitaani. Gaddafi anatishia usalama wa WaLibya kwa mamilioni kwa kila siku anayoendelea kuamka akiwa madarakani.
Tushukuru , kuwa Gaddafi hana silaha za kemikali wala nyuklia, maana, Gaddafi wa sasa, katika dakika za mwisho za kupoteza mamlaka, angeweza kufanya maangamizi makubwa kwa WaLibya na dunia. Kisingizio? Njama za Wazayuni, George Bush ( hata kama hayupo madarakani) na Osama bin Laden! Je, kuna namna nyingine ya kumtambua kama binadamu ni mwendawazimu?

Kwa sasa Gaddafi ametengwa na dunia na hata baadhi ya marafiki zake. Huenda Gaddafi yuko tayari kufanya lolote lile kwa sasa, maana, hajui ni wapi salama pa kukimbilia. Hata kwa rafiki yake Mugabe kuna wanaojiandaa kufanya kama ya Tunisia na Misri.
Na kule Saudi Arabia? Haiwezekani. Si ana ugomvi wa siku nyingi na mfalme. Na wala Gaddafi asingepata tabu sana kupata pa kukimbilia, lakini, ugumu anaoupata sasa ni wa kujitakia; kuwaua watu wake. Hata rafiki zake wanapata tabu kumwelewa kwa hilo, maana, wao bado wana chembe za aibu.Naam. Kiongozi wa nchi haui watu wake, Gaddafi amewaua, hana aibu. Na hilo ni Neno La Leo.
Maggid
Iringa
Jumapili, Februari 27, 2011
Maggid
Iringa
Jumapili, Februari 27, 2011
No comments:
Post a Comment