Mtoto wa kituo cha Rafiki Child Care Home kilichopo Mererani wilaya Simanjiro mkoani Manyara Anna Lameck akipokea vifaranga vya kuku kutoka kwa Mkurugenzi wa Vodacom kanda ya kaskazini Nguvu Kamando mara baada ya kukabidhiwa rasmi na Vodacom Foundation mradi wa ufugaji kuku kwa kituo hicho,Mradi huo umegharimu shilingi Milioni 15.
kwa picha zaidi Bofya Read More
kwa picha zaidi Bofya Read More
Mkurugenzi mahusiano wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba akimkabidhi kifaa cha kulishia vifaranga vya kuku mtoto wa kituo cha Rafiki Child Care Home Nehemia Justin,kituo hicho kilichopo Mererani wilaya Simanjiro mkoani Manyara,Mfuko huo umetoa msaada wa jengo la kufugia kuku vyote vikiwa na thamani ya Milioni 15,anaeshihudia ni Mkurugenzi wa Vodacom kanda ya kaskazini Nguvu Kamando.
Mkurugenzi wa Vodacom kanda ya kaskazini Nguvu Kamando , Mkurugenzi mahusiano wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba na Mtoto aishie katika mazingira magumu wa kituo cha Rafiki Child Care Home cha Mererani Miriam Muya wakiweka vifaranga vya kuku kwenye banda mara baada ya kukabidhiwa msaada wa mradi huo wenye thamani ya shilingi Milioni 15.
Mkurugenzi mahusiano wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba akijadiliana jambo na Meneja wa Vodacom kanda ya kaskazini Henry Tzamburakis walipofika katika kituo cha Rafiki Child Care Home cha Mererani kutoa msaada wa mradi wa kuku, mradi huo una thamani ya shilingi Milioni 15.(picha kwa hisani ya Haki Ngowi)
No comments:
Post a Comment