ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, March 1, 2011

Aliyemzalisha mtoto wa miaka 11 asakwa

Image

Na sifael paul
Sakata la mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Narida anayekadiriwa kuwa na miaka kati ya 35 na 40, anayetuhumiwa kumzalisha binti wa miaka 11, Nangatikwa Lowassa, limechukua sura mpya.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, ameingilia kati akitaka mtuhumiwa asakwe na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Waziri huyo amesema kuwa, kitendo alichofanya mwanaume huyo mkazi wa Ngarananyuki mkoani Kilimanjaro ni kosa la jinai hivyo kuliagiza jeshi la polisi kufanya kazi yake.

Katika tukio hilo, Nangatikwa kutoka jamii ya Kimasai iliyoko wilayani Siha mkoani Kilimanjaro, aliwashangaza wengi baada ya kujifungua bila kupata tatizo lolote, licha ya umri mdogo alionao huku baadhi ya watu wakihoji uwezekano wa jambo hilo Kibaolojia.

Akizungumza muda mfupi baada ya kujifungua katika wodi ya wazazi ya Hospitali ya Wilaya ya Hai iliyoko Machame alikolazwa baada ya kuugua Malaria mara baada ya kujifungua, binti huyo alisema haoni
na wala hakupata tatizo lolote kwa yeye kujifungua mtoto na hata kuwa na mume.

Binti huyo alisema aliachishwa shule na kuolewa mwaka jana ambapo kwa sasa anaishi na mume wake Narida.

Kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa ya 1971, inayopingwa na wanaharakati, mtoto wa kike anaweza kuolewa akiwa na umri wa miaka 14, lakini baada ya wazazi kuafiki achukue hatua hiyo.

Hata hivyo, sheria hiyo inapingana na ile ya Makosa ya Kujamiiana ya 1998, ambayo imeeleza wazi kuwa mtoto yeyote chini ya miaka 18 akiingiliwa kimwili atakuwa amenajisiwa.

CHANZO:GLOBAL PUBLISHERS

No comments: