Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Tekonolojia, Charles Kitwanga
ZAIDI ya asilimia 90 ya Watanzania watakuwa wamefikiwa na huduma ya mawasiliano ya simu ifikapo mwaka 2013, Bunge lilielezwa jana.
Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Tekonolojia, Charles Kitwanga alisema kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa upatikanaji wa huduma za mawasiliano nchini kote kwa kiwango kinachoridhisha.
Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Tekonolojia, Charles Kitwanga alisema kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa upatikanaji wa huduma za mawasiliano nchini kote kwa kiwango kinachoridhisha.
Hata hivyo alisema jambo linalokwamisha mchakato huo mara nyingi huwa ni maeneo ya Kijiografia ambayo yanakwenda sambamba na idadi ndogo ya watu katika maeneo husika ambako hakuwiani na gharama kubwa za uwekezaji.
Katika swali la msingi, Mbunge wa Kondoa kusini , Zabein Mhita(CCM) alitaka kujua Serikali itawapatia lini mawasiliano ya simu wananchi wa Kata za Kingale, Suruke, Serya, Hondomario, Changea,Thawi, Soera, Kikilo na Busi ambayo hayana mawasiliano kabisa.
Waziri alisema uhaba wa miundombinu ya barabara na nishati ya kutosha yenye gharama nafuu kwa ajili ya kuendeshea mitambo ya mawasiliano ni kikwazo kikubwa kwa kampuni za simu kufikisha huduma ya mawasiliano katika maeneo husika.
Akizungumzia suala la ujenzi wa mawasiliano katika Wilaya ya Kondoa, Naibu waziri alisema Kampuni ya Airtel imeyaweka maeneo hayo kwenye mpango wake wa tathimini yakinifu katika muhula wa nne wa utafiti wa mwaka 20011 ili hatimaye iweze kuwapatia mwasiliano wananchi wa maeneo yaliyotajwa na Mbunge.
Alisema katika kutekeleza jambo hilo,pia mfuko wa mawasiliano tayari umeainisha jumla ya vijiji 11 vyenye eneo la ukubwa wa kilomita 1,793 katika Mkoa wa Dodoma.
Aidha alisema tayari kampuni ya simu ya TTCL imeahidi kuyaweka maeneo ya Wilaya ya Kondoa katika mkakati wa mwaka 2011/13 ambao utekelezaji wake unategemea upatikanaji wa fedha.
CHANZO:MWANANCHI
No comments:
Post a Comment