ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 14, 2011

Majambazi wavamia Muhimbili, waua na kupora Sh25 milioni

Hadija Jumanne
WATU wanaoaminika kuwa majambazi wamevamia Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), kumuua mlinzi na kuiba Sh12.5 milioni.Licha ya na kumuua Juma Breshi wa Kampuni ya Ulinzi ya Full Time Security, walimjeruhi kwa risasi mfanyakazi wa hospitali hiyo, Sabina Masawe, kabla ya kupora fedha hizo.

Habari zilizofikia gazeti hili zimeeleza kuwa, tukio hilo lilitokea saa 2:15 asubuhi jana.Kwa mujibu wa habari hizo, majambazi hao wakiwa na pikipiki, walivamia gari ya hospitali hiyo iliyokuwa imebeba fedha kutoka Kitengo cha OPD kwenda ofisi za Idara ya uhasibu hospitalini hapo, ili baadaye zipelekwe benki.

Ofisa Uhusiano wa Hospitali ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha, alisema tukio hilo lilitokea jana eneo la chumba cha kuhifadhia fedha.Kwa mujibu wa Aligaesha, fedha hizo zilikuwa za makusanyo ya siku tatu kuanzia Ijumaa iliyopita hadi Jumapili.“Ni kweli tukio hilo limetokea leo (jana) na mlinzi mmoja wa Kampuni ya Fulltime ambaye alikuwa akisindikiza gari hilo, ameuawa kwa kupigwa risasi,” alisema Algaesha na kuongeza:"Majambazi hao walivamia gari la fedha lilipokuwa linatoka Kitengo cha OPD kuelekea ofisi za idara ya uhasibu."Alisema baada ya kuvamia gari hilo, walimpiga risasi ya kwapa la kushoto mlinzi huyo na mfanyakazi wa kitengo cha maabara ambaye alipigwa risasi kwenye baja la mguu wa kulia.
Alisema mfanyakazi huyo alipigwa risasi wakati akivuka kwenda kuchukua vitafunwa.Aligaesha alisema mlinzi huyo alikuwa ameongozana na gari lililokuwa na fedha ambalo lilikuwa na watu wanne.”Miongoni mwao ni wahasibu wawili na dereva mmoja.
Walipofika ofisi za uhasibu, walishuka, lakini kabla hawajaondoka walishtushwa na mlio wa risasi mbili,” alisema.Alisema haikufahamika mara moja sehemu walikokuwa wamejificha majambazi hao wakati gari hilo lilipowasili, lakini walipiga risasi mbili ambazo zilivunja kioo cha gari na kumpiga mlinzi huyo na nyingine kumpiga mfanyakazi wa kitengo cha maabara aliyekuwa akipita eneo hilo.Alisema baada ya tukio hilo, majeruhi huyo alikimbizwa hospitalini hapo na kulazwa.

Akizungumza kwa taabu, majeruhi huyo alisema alikuwa akielekea kununua vitafunwa, ghafla wakati anavuka, akashtukia amepigwa na kitu paja lake la kushoto.”Sikuweza kujua mara moja nimepigwa na nini. Nilishangaa kuona baja linatoka damu nyingi na nikashindwa kutembea kutahamaki, nikasikia kelele za watu na baada ya hapo sikuelewa kilichoendelea tena mpaka sasa ndiyo nimeshtuka,” alisema.
Ofisa Muuguzi wa Mapokezi ya Dharura, Victoria Mlele, alisema majeruhi huyo alipelekwa katika chumba hicho kwa maandalizi ya awali, ili kupelekwa Taasisi ya Mifupa (Moi) kufanyi wa upasuaji ili kutoa risasi hiyo. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, alisema hana taarifa zozote kuhusu tukio hilo.Mwisho

No comments: