ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 14, 2011

SHUKRANI ZA DHATI

Bi Rehema Barksdale na familia yake wanatoa shukrani zao za dhati kwa kumuunga mkono katika matembezi ya "Breast Cancer Race for the Cure" yaliyofanyika Washington, DC tarehe o6/04/11 na kwa msaada na ushirikiano wenu. Kuitikia kwenu na kujitokeza kwenu ndiko kulikofanikisha shughuli hii. Bila yenu tusingefikia lengo ambalo tumelifikia.
Pia wanatoa shukurani kwa wote walioacha shughuli zao na kujumuika pamoja nao katika maulid yaliyofanyika siku iliyofuata ya jumapili. Hana cha kuwalipa ila Mwenyezi Mungu ndiye atakayewalipa na kuzidi kuwapa moyo wa ushirikiano.
Cha muhimu katika yote haya ni kukumbuka kuwa magonjwa haya ya saratani (cancer) - iwe ya maziwa (breast), mapafu (lungs), damu (Leukemia), kizazi (ovarian) na kadhalika, pamoja na magonjwa mengine kama vile pressure, kisukari n.k, yanatibika na kuna sehemu nyingi ambazo wanatoa misaada ya bure katika kinga na matibabu yake. Ni vizuri tukiweza kueleweshana wapi pa kwenda na nini cha kufanya kuweza kujikinga na kupata matibabu hapo yanapohitajika. Nakuombeni tuendelee kuwa pamoja katika kueleweshana na kusaidiana wakati wote.

AHSANTENI SANA!

No comments: