Timu ya taifa ya soka ya wanawake, Twiga Stars, imealikwa kushiriki katika mashindano ya mwaka huu ya Kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara (COSAFA) yatakayoanza Julai 2 nchini Zimbabwe.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah, alisema kuwa shirikisho limethibitisha kuipeleka Twiga Stars kwenye mashindano hayo ili yawe kama sehemu ya maandalizi ya kushiriki kwenye Michezo ya Afrika 'All Africa Games' itakayofanyika baadaye mwaka huu.
Osiah alisema kuwa timu hiyo iliyokuwa ikifanya mazoezi yake kwa wachezaji kutokea nyumbani, sasa itaingia kambini wakati wowote kuanzia leo baada ya kupokea mapendekezo kutoka kwa Kamati ya Ufundi.
"Kwa muda mrefu timu hiyo ilikuwa inafanya mazoezi yake kwa mtindo wa wachezaji kutokea nyumbani ambapo tunawapa posho na nauli kidogo ya kujikimu, hawakuwa wamelala baada ya kufuzu," alisema katibu mkuu huyo.
Alisema wanaamini kwamba mashindano hayo yanayoshiriki nchi za Zimbabwe, Afrika Kusini, Namibia, Msumbiji na Swaziland, yatawaimarisha na kuwasaidia kwenda kwenye michezo ya Afrika wakiwa imara.
Twiga Stars ambayo mwaka jana ilifuzu kwa mara ya kwanza kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake zilizofanyika Afrika Kusini, mwaka huu imekata tiketi ya kucheza fainali hizo la All Africa Games zitakazochezwa Maputo, Msumbiji mwezi Septemba 'kiulaini' baada ya wapinzani wao Sudan kujitoa katika siku chache kabla ya mechi yao.
Hata hivyo, Twiga Stars ambayo iko chini ya kocha mzalendo, Boniface Mkwasa anayesaidiana na Mohammed Adolph, mwaka jana nchini Afrika Kusini ilifanya vibaya na kuishia kwenye hatua ya makundi kutokana na kufungwa mechi zake zote tatu ambapo ilikuwa kundi moja na wenyeji (Banyana Banyana), Mali na waliokuja kuwa mabingwa, Nigeria.
CHANZO: NIPASHE
1 comment:
Hey..
Nice Article, clear and detailed description...
Thanks a lot for sharing the information.....
By the way check the latest information about the All Africa Games 2011 here, like events, programs from All Africa Games 2011.
Post a Comment