Pascal Issa Amri akiwa Hospitali ya CCBRT wodi ya Mifupa baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondolewa mfupa wa ziada uliomtesa kwa miaka 17 akiwa ameshika kikopo kilichohifadhiwa mfupa uliondolewa ambao umepelekwa Hospitali ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.
(www.mohammeddewji.com/blog)Na.Mwandishi wetu.
Zoezi la upasuaji wa kuondoa mfupa wa ziada kwa Kijana Pascal Issa ambalo liliendeshwa mwanzoni mwa wiki hii, limefanikiwa na kwamba Pascal anaendelea vizuri na amelazwa katika hospitali ya CCBRT JIJINI Dar es salaam.Pascal ambaye alilazwa Jumapili baada ya kupata msaada kutoka kwa Bw SALUM AWADHI na hospitali hiyo ya CCBRT anaendelea vizuri na mfupa uliondolewa umepelekwa katika hopsitali ya Taifa ya Muhimbili kwaajili ya uchunguzi zaidi.
Kwa upande wa Madaktari waliendesha upasuaji huo uliochukua Saa NNE wamesema, upasuaji huo umefanyika kwa mafanikio makubwa na kwamba Pascal ataendelea kubaki hospitali hapo kwa uangalizi zaid mpaka atakapojiskia vizuri sambamba na kusubiri majibu ya Mfupa huo uliotolewa .
No comments:
Post a Comment