Advertisements

Tuesday, December 20, 2011

Uturuki yajipanga kuanza safari za ndege Zanzibar

Tali Ussi  Zanzibar
BALOZI wa Uturuki anayemaliza muda wake wa kufanyakazi nchini,Sander Gurbuz imesisitiza azma ya Shirika la Ndege la Uturuki kuanza safari kati ya nchi hiyo na Zanzibar.

Balozi huyo amesema azma hiyo iko pale pale na kwamba utekelezaji wake unaweza kuanza hivi karibuni lengo likiwa ni kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
 
Aiyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na Rais wa Zanzibar,Dk Ali Mohamed Shein,  Ikulu mjini Zanzibar.Balozi Gurbuz alisema tayari ndege za shirika hilo zimeshaanza kutoa huduma kati ya Uturu na Tanzania Bara na kwamba mkakati uliopo sasa ni kuanza safari za kwenda Zanzibar.


Alisema safari za ndege hioyo katika visiwa vya Zanzibar, zitaimarisha pia  sekta ya utaliii kutakakosababishwa na ongezeko la watu kutoka Uturuki.

Alisema pamoja na mpango wa kuanzisha safari za ndege, nchi yake pia itaendelea kushirikiana na Zanzibar katika sekta mbalimbali za maendeleo.
 
Katika mazungumzo hayo, Balozi Gurbuz alisema uhusiano kati ya Uturuki na Tanzania umeendelea kuimarika siku hadi sikui.Kwa upande wake, Dk Shein ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar, alimpongeza balozi huyo kwa juhudi zake katika kufanyakazi za kuiwakilisha vema nchi yake.

Pia alipongeza ushirikiano mzuri ulipo kati ya Tanzania na Uturuki na kutaka uendelezwe kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizi mbili.

No comments: