Advertisements

Tuesday, December 13, 2011

WATANZANIA WASHEREHEKEA MIAKA 50 YA UHURU UGIRIKI

Keki ya sherehe za  Miaka 50 ya UHURU Tanzania Bara, zilizofanyikia Ofisi za Balozi wa Tanzania mtaa wa Lemesoy uliopo Athens, Ugiriki.sherehe hizi zilisherehekewa kwa shangwe na burudani na miongoni mwa matukio yaliyovutia zaidi ni sinema ya jinsi wakoloni wa Uingereza walivyokabidhi madaraka kwa viongozi wa Nchi siku ya 9 December, 1961
Namba zinazoashiria miaka 50 ya UHURU wa Tanzania Bara zinavyowaka na kumeremeta kweli ni tukio la kihistoria kwa Watanzania wa Ugiriki, Nyumbani na kwa Watanzania wote Duniani. 
Watanzania wa Ugiriki wakijumuika pamoja kusherehekea miaka 50 ya UHURU ilyofanyikia Ofisi za Ubalozi wa Tanzania zilizopo mtaa wa Lemesoy jijini Athens, Ugiriki.
Eddy Islam akipata picha ya pamoja na Mzee wa Kitanzania anaeishi Jiji hapo katika sherehe za miaka 50 ya UHURU iliyofanyikia kwenye ofisi za Ubalozi wa Tanzania Athens, Ugiriki.
Watanzania wa Ugiriki wakijumuika pamoja katika sherehe za miaka 50 ya UHURU wa Tanzania Bara,hapa wakipata picha ya pamoja kwenye keki ya UHURU na Bendera ya Tanzania kama moja ya ukumbusho wa sherehe hizo za kihistoria.
Katika kusherehekea miaka 50 ya UHURU Watanzania wa Ugiriki walicheza michezo mbali mbali ikiwemo pool kama uonavyo Watanzania hawa.
Watanzania wa Ugiriki wakijumuika pamoja kusherehekea miaka 50 ya UHURU wa Tanzania Bara,hapa wakipata picha ya pamoja

No comments: