ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, January 4, 2012

Hatma ya Hamad Rashid na wenzake kujulikana leo

Baraza Kuu la Chama Cha Wananchi (CUF) leo linakutana mjini Zanzibar kisikiliza utetezi wa Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed na wenzake 14, ambao wanatuhumiwa kwa kusababisha mgogoro katika chama hicho.

Wajumbe wa kikao hicho walianza kuwasili Zanzibar tangu jana tayari kwa ajili ya kikao hicho ambao kitatoa hatma ya viongozi hao, ambao tayari wamehojiwa na Kamati ya Nidhamu na Maadili.
Wakati huo huo, CUF Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, kimewashauri  wajumbe wa Baraza Kuu kutumia katiba ya chama wakati  watakapokutana leo.
“Kubwa zaidi ni kusigana kwa kauli kati ya Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad na Sekretarieti ya chama kwa upande mmoja na Hamad Rashid kwa  upande mwingine,” alisema  Kaimu Katibu wa CUF Wilaya ya Nyamagana, Hamduni Marcel wakati akizungumza na wandishi wa habari jana.


Alisema ni vema Baraza likafikia uamzi utakaokiimarisha chama kwa kuzingatia katiba na busara za wajumbe.
Marcel  alishauri Baraza litumie uzoefu  na uvumilivu wa mfumo wa chama ambao katika  miaka  kadhaa iliyopita ulisaidia kufikia mwafaka kati ya CUF na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kwa mujibu wa Marcel, mgogoro  unaofukuta unatokana  pia na makovu ya Uchaguzi Mkuu  uliopita
CHANZO: NIPASHE

No comments: