Ndugu Watanzania na Wote wapendao Kusali kwa Lugha ya Kiswahili. Nawakumbusha kuwa Misa kwa Lugha ya Kiswahili itafanyika:- Jumapili Januari 8, 2012 Saa 8 mchana. MAHALI:- Kanisa la Mt. Edward 901 Popoar Grove St. Baltimore, MD 21216 Baada ya Misa Karibuni wote kwenye ukumbi wa Parokia kwa Viburudisho na Chakula. |
Maelekezo ya Kuegesha Magari:-
Tunayo sehemu ya kuegesha lakini ni kidogo kama magari 10 tu. Iko Prospect St. karibu na kanisa. Kuna nafasi kubwa zaidi ya kuegesha kwenye Shule ya Msingi "Alexander Hamilton" inayotazamana na Kanisa. Usiogope usalama utakuwepo. Nimewaomba polisi wawe wanapitapita kipindi chote cha Noeli na Mwaka Mpya.
Kumbuka Ni Maadhimisho yetu ya Noeli / Krismasi na Mwaka mpya kwa mpigo.
Ni siku pia ya kuliombea Taifa Letu kwani Misa yetu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru hatukuweza kuiadhimisha kama tulivyotarajia. Tutawaombea ndugu zetu waliokumbwa na mafuriko na wale walioumizwa kwa Mabomu. Walio na Maombi maalumu tutayatolea Pia.
Tutaadhimisha Misa ya sikukuu ya Epifania:-
Masomo:-
1. Somo katika Kitabu cha Nabii Isaya 60:1-6
2. Wimbo wa Katikati: Zaburi 72: 1-2; 7-8; 10-13 Kiitikizano :- Mataifa yote ya Ulimwengu watakusujudia, Ee Bwana.
3. Waraka wa Mtume Paulo wa Waefeso:- 3:2-3, 5-6
4. Injili ya Mt. Matayo 2:1-12
Nyimbo:-
Ø Nimeonja Pendo lako
Ø Nyota nzuri yenye Ajabu
Ø Karibu Moyoni mwangu Bwana (Komunyo)
Ø Kwa vigelegele na Shangwe
na Mungu Ibariki Afrika na Tanzania.
Yeyote Anayesoma Tangazo hili naomba utusaidie kuwapa taarifa wengine. Asante sana.
Padri Shao
No comments:
Post a Comment