ANGALIA LIVE NEWS
Monday, January 16, 2012
mkufunzi wa kimataifa ,Josef Diouf kutoka Shirikisho la masumbwi Dunia (AIBA) atua nchini
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKISHO la Ngumi za ridhaa nchini (BFT) limepiga panga majinamatano kati ya 5 ya makocha walioteuliwa kushiriki katika kozi yakimataifa ya mchezo huo iliyopangwa kufannyika kesho Januari 16 mwaka huu.BFT imewakata washiriki hao baada ya Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC)kuwataka BFT kupunguza idadi ya washiriki kutokana na hasarailiyosababishwa na washiriki hao katika kozi ya awali iliyokuwaifanyike tangu mwezi Novemba mwaka jana.TOC ambayo huandaa kozi za michezo mbalimbali kutokana na ruzukuinayotolewa na Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC) ilikuwa iendeshekozi hiyo tangu mwaka jana lakini haikufanyika kutokana na mkufunzi wakozi hiyo kutoka nchini Algeria kuingia mitini, Kozi hiyo ya Kimataifa ya Mchezo wa masumbwi kwa mara ya mwisho ilifanyika nchini mwa 2002 ambapo ni ngazi ya juu kabisa ya ukocha Duniani kote
TOC ililazimika kuwalipa nauli baadhi ya washiriki waliotoka nje yaDar es Salaa kutoka katika fungu la pesa za kuendeshea kozi hiyohivyo kuwataka BFT kupunguza idadi ya washiriki hasa wale waliofanyautovu wa nidhamu katika kozi ya awali ili kiwango cha pesa kilichobakikutosheleza mahitaji wa kozi itakayoendeshwa Januari 16 mwaka huu.Akizungumza Dar es Salaam Katibu mkuu wa BFT, Makore Mashaga alisemaidadi ya makocha 25 waliowateua inaweza ikapungua tena kulingana nabajeti waliobaki nayo TOC ambapo hata hivyo hakuyataja majina matanoya washiriki walioachwa .Aliwataja washiriki waliopenya kuhudhuria kozi hiyo ni mpiga picha waMagazeti ya Busines Time, Majira, Sports Starehe na Jarida la Maishaambaye pia alikuwa bondia, Rajabu Mhamila 'Super D', Anord Ngumbi,Moses Lema, Anthon Mwang'onda na Edward Emanuel (Dar es Salaam).Wengine ni Yahaya Mvuvi (Tabora), Joseph Mayanga na Zakaria Mwaseba(Morogoro), Omari Saady na Mussa Bakari (Mwanza), Ally Ndee (JKTMbeya), Emilio Moyo na Gaudens Uyaga (Pwani) Juma Liso (MagerezaKigoma), Lyinda Kalinga (Dodoma) na Abdalah Bakari (Tanga).Wengine ni Mohamed Hashim (Polisi Dar es Salaam), David Yombayombam,Haji Abdalah, Said Omari (JWTZ), Mazimbo Ally, Rogated Damian naFatuma Milanzi (JKT), Musa Maisori na Hamisi Shaaban (Magereza Dar esSalaam).Kozi hiyo itaendeshwa na mkufunzi wa kimataifa Josef Diouf kutokaShirikisho la Dunia la mchezo huo (AIBA) ambaye atashirikiana namakamu wa Rais wa BFT, Michael Changarawe.Kozi hiyo itafanyika latika shule ya Sekondari ya Filbert Bayi KibahaMkoani Pwani na itafikia tamati Januari 24 mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment