ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, January 3, 2012

SHUKRANI ZA DHATI


FAMILIA YA STEINA MREMA NA MARAFIKI NA KAMATI ILIYOKUA IKISAIDIA KUKUSANYA PESA ZA KUSAFIRISHA MWILI WA MPENDWA WETU, MTANZANIA MWENZETU NA RAFIKI YETU MKUBWA STEINA KWA MAPUMZIKO KWENYE NYUMBA YAKE YA MILELE, TANZANIA.


INATOA SHUKRANI ZA DHATI KWA WOTE WALIOJITOLE KWA HALI NA MALI NA HATIMAE KUWEZESHA KUMSAFIRISHA MAREHEMU TANZANIA.


MWILI WA MAREHEMU ULIONDOKA JUMATATU JANUARY 2, 2012 UKISINDIKIZWA NA MAMA MTOTO NA MTOTO WA MAREHEMU NA UNATARAJIWA KUFIKA KILIMANJARO (KIA) SIKU YA JUMATANO JANUARY 4, 2012 SAA 5:30 SAA ZA TANZANIA NA KLM


KUSEMA UKWELI HATUNA CHA KUWALIPA  KITAKACHOLINGANA NA HAYO MAKUBWA MLIOFANYA, USHIRIKIANO, MSHIKAMANO NA MOYO WA UPENDO MLIOUNYESHA BILA KUJALI MAJUKUMU MAKUBWA YANAYO WAKABILI NCHI HII MLIWEZA KUJIKUNA PALE MSIPOFIKIA ILI MRADI KUWEZESHA KUMSAFIRISHA MWENZETU, NDUGU YETU, MPENDWA STEINA MREMA.


MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA AWAANGAZIE NA AWAZIDISHIE MARA ELFU.


ASANTENI SANA NA MUNGU AWABARIKI

4 comments:

Anonymous said...

poleni sana wafiwa... nimesikia tetesi kuwa dada yake kwize naye kafiwa na mwanae, je, habari hizi ni za ukweli? na nimtoto yupi? naomba utupe taarifa tafadhali dj luke

Anonymous said...

Jamani ya ngoso mwachie ngoso hata ukiambiwa,huna lolote sana sana chokochoko,wewe usiyokuwa na haya kutaka kujua tu ya watu.jamani dj luke embu toa tena neno maana watu tunaogopa hata kuwakaribisha watu majumbani sababu ya tabia za ajabuajabu watu unawakaribisha wakitoka tu mimi pale vile huku vile mbona binadamu hatupendani unafiki mtupu tena unakuta wale uliowapa kipaumbele kama rafiki zako wa karibu wapo mstari wa mbele kukutangazia hii inakuwaje ,jitu halikujui ila linavyokuchambua utadhani mmezaliwa pamoja.Tuheshimiane jamani,mtu kukuita kaka ,dada,uncle,Aunt,sister ni heshima.

Anonymous said...

mdau punguza jazba. mtu kauliza swali wewe unatuandikia insha, obvious u r the one with chokochoko

Anonymous said...

wewe mwanamke ulieandika ya ngoswe muachie ngoswe inahusiana nini humu katika blog?maana hakuna mwanaume mwenye muda mchafu wakuandika upupu wa aina hii.. na wewe luke, mtu kama huyu unatoa post yake ya nini? mdau kauliza swali tena kwa wema tu, cheki guberi lilikotokea na kujibu upupu hapa ktk blog yako.. yani huyu kama haitwi shida, basi anaitwa sikuzani au matatizo, maana lazma nikuku la kienyeji hata kusoma na kuelewa halielewi.. huku marekani sijui linafanya nini wallah, naona keshawakosha wazee yakutosha sasa vile vinyesi vimemungia hadi kwenye medula oblongata yake na ndio maana reasoning imekuwa zero..!!
by the way mdau, ni kweli chimpae kafiwa na mwanae tanzania na wanaenda huko hivi karibuni kwa ajili ya mazishi.. haya we bi sikuzani leta maneno nikuwashe sasahivi..!! acha kuwa na akili kama mende wewe..!! JIHESHIM MTU WANGU..!!