Watoto wa wateja wakicheza
Wana Twanga wakiburudisha
Operations Manager, MultiChoice Tanzania, Ronald Shelukindo akimkabidhi Jane Mhina wa Hotspot Media HD PVR aliyoshinda kwenye draw wakati wa siku hii maalumu kwa wateja wa DStv.
Kampuni ya Multichoice Tanzania jana iliwakaribisha wateja wake wote kwaajili ya siku maalum ya kuzungumza nao ili kujua kero zao na pia kupata ushauri wa jinsi ya kuwahudumia vizur zaidii. Pamoja na kuzungumza nao pia kulikuwa na matukio mbali mbali kama michezo mbali mbali ya watoto na burudani ya mziki iliyoporomoshwa na bendi ya African Stars Twanga Pepeta.
Pia kulikuwa na draw mbali mbali ikiwepo ile iliyomuwezesha mteja mmoja kujishindia Dikoda ya HDPVR na wengine kujishindia malipo ya mwezi. Wadau mbali mbali walihudhuria wakiwemo Airtel Money,Tigo Pesa,NMB Mobile,Selcom Wireless ambao wote hawa ni wadau wakubwa wa wateja wa DStv kwani malipo ya wateja hupitia kwenye mitandao yao na huduma hurudishwa mara moja.
No comments:
Post a Comment