NI matumaini yangu kuwa mpo kamili katika shughuli za ujenzi wa taifa, lakini ili kunogesha mihangaiko yetu tupate mwendelezo wa mada yetu kutoka pale tulipoishia wiki iliyopita juu ya makosa ambayo hatutakiwi kuyafanya kwenye uhusiano wa kimapenzi.
Jambo la kutambua ni kuwa hilo ni moja kati ya makosa makubwa ambayo watu huyafanya katika uhusiano wa kimapenzi.
Katika kosa la maigizo, wengine huamini mpaka nguvu za giza. Kwamba mtu anabadilisha waganga ili kuteka hisia za mtu. Muhimu ni kutambua kuwa hakuna mganga wala mchawi anayeweza kuufanya uhusiano wako uwe na afya.

Achana na maigizo, jiamini na uache mguso wako wa asili ndiyo umvute. Wengi wanaoendeshwa na kujivika uhusika ambao hawana ni washamba wa mapenzi. Hata kama baadhi hufanikiwa kutimiza matarajio yao mwanzoni lakini mwisho hubaki na aibu.
KUZIDIWA NA HISIA MAPEMA
Jambo lingine ambalo ni hatari kubwa ni kuzidiwa na hisia mapema. Hakuna anayeweza kupinga ukweli kuwa mapenzi ni mchezo wa hisia, kwa hiyo siyo kosa kuzionesha kwa mtu ambaye umempenda. Tatizo ni wakati wa kuzionesha. Haifai kuzidiwa mwanzoni mwa uhusiano.
Ikae akilini kwako kuwa maisha ya sasa, mpaka unakuja kukutana na mwenzi wako, utakuwa umeshapita kwa wengine, naye ni hivyohivyo, kwa hiyo kila mmoja anajua matarajio ya mapenzi. Kitendo cha kuzidiwa na hisia huamsha hali fulani ya usumbufu kwa mwingine.

Nitoe msisitizo kuwa watu wazuri kwenye mapenzi ni wachache lakini wanatolewa macho na wengi. Kwa kulitambua hilo, unapaswa kuishi kwa akili ili usigeuke kero. Endapo atakuona msumbufu, hatasita kumkaribisha yule ambaye anamuona atampa furaha badala ya karaha.
Lazima atakuwa na uzoefu wa kimapenzi, bila shaka anaujua utulivu katika uhusiano. Kama ndivyo, unadhani atakubali kupoteza muda kwako, wakati kila siku unachemsha kichwa chake kwa maswali au vitendo ambavyo chanzo chake ni kuzidiwa na hisia za mapenzi juu yake?

Ieleweke kuwa hisia hutokana na ukweli wa mapenzi. Yaani, unapozidiwa na hisia, maana yake moyo wako haudanganyi. Unapenda kupitiliza, kwa hiyo unakuwa unahitaji na mwenzako naye akutendee haki. Ni hapo ndipo usumbufu huibuka. Upendo hugeuka kero kwa anayependwa.
Mapenzi siyo maneno, vitendo ndiyo hutafsiri upendo. Vema ukatia akilini kuwa kama kweli unampenda, utamsaidia pia kupata utulivu. Wewe ndiye utamfanya awe na utulivu, endapo hutampa usumbufu wa hapa na pale. Inahitaji busara kidogo kulitambua hilo, kwani wengi wamefeli.

Mara nyingi mtu anayezidiwa na hisia, hushindwa kujidhibiti. Mwenzi wake akichelewa kujibu SMS, hugeuka tatizo kubwa linalohitaji suluhu ya mtu wa tatu. Akimpigia simu, ikaita mara saba bila kupokelewa, akipokea tu shari. Kabla ya salamu ni swali: “Mbona hupokei simu?”
Katikati ya mazungumzo, kama upande wa pili utaonekana kuna utulivu, shari inaanza: “Mbona upo sehemu iliyotulia hivyo? Upo wapi?” Kwa akili ya haraka, inamtuma mwenzi wake yupo nyumba ya kulala wageni, hoteli au sehemu yoyote akishiriki tendo la faragha na mtu mwingine.

Hisia mara nyingi hudanganya, kwani huzalisha mawazo mabaya na matokeo yake ni karaha ndani ya uhusiano. Hakuna anayeweza kuvumilia tuhuma za kila mara. Mapenzi maana yake ni amani na furaha, wewe hiyo amani humpi, furaha ndiyo hana kabisa. Lazima atakukimbia au atakuumiza zaidi kwa sababu anaweza kutafuta mlango wa kutokea wakati hujajiandaa kuachwa.
Itaendelea wiki ijayo.
www.globalpublishers.info
1 comment:
ni kweli uliyoeleza lakin kila mtu anaupendo wake iweje leo umpende mtu ukazidiwa na yeye hakuonyeshi chochote si ndo balaa hii na ndo unaaza kujiuliza hivi kweli ananipenda au anataka kunipotezea muda wangu, na usisikiye hakuna ujuzi wala utaalamu ukizidiwa umezidiwa, mulize mzee yussuf kwenye nyimbo yake ya taarab ukizidiwa huna ujaanja bro hata kama unautulivyu na ukiwa naupendo wa kweli lazima ukimpigia mwenzio simu hapokei utataharuki wee acha hizo aisee.
na iweje kila mwenzio akikupigia wewe unampokelea yeye ukimpigia hapoke zaidi ya mara kumi na una tegema kwamba nikimpata nimwambi maneno mataa tama ya asali, wee acha hizo
kama hujui mampenzi basi ndo hayaaa na kama unapenda kweli lazima utakuwa na jazba mwenzio akikuleta za kuleta za kitoto.
salaam hizi zime toka New York china town
(from mtanzania wa macho ndogo/mchina)
Post a Comment