Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) kimepokea nakala ya hukumu ya kesi mbili zilizofunguliwa Marekani
dhidi ya mbunge wa Viti Maalum Leticia Nyerere (CHADEMA) zenye kuonyesha mahakama
imetupilia mbali kesi hizo. (Rejea Kiambatanisho).
Kwa mujibu wa mbunge wa Viti Maalum
Leticia Nyerere waliofungua kesi hiyo waliingia mitini baada ya kubainika kwa
tuhuma kwamba kesi hiyo ilikuwa ni ya kutengenezwa kwa malengo ya kumchafua
hali ambayo ingeweza kuwatia hatiani wahusika kwa kuwasilisha madai ya uongo.
Pamoja na kutupiliwa mbali kwa kesi
hizo mamlaka husika za Marekani zinaendelea na uchunguzi wa kumsaka aliyetoa
madai kwamba Mbunge Leticia Nyerere amekamatwa na kutaka wananchi wamchangie
fedha kwenye akaunti iliyotajwa katika ujumbe uliosambazwa kwa njia ya mtandao.
Hukumu hii inadhihirisha tahadhari
niliyoitoa kwa wanahabari tarehe 17 Mei 2012 ya kuwataka kusubiri maelezo rasmi
kutoka kwa Leticia Nyerere na yatokanayo mahakamani kutokana na tuhuma
zilizosambazwa kwenye mitandao kuwa na mwelekeo wa siasa chafu kukwaza jitahada
zake na viongozi wa CHADEMA kutokana na
kazi walizozifanya za kuwezesha watanzania waishio Marekani kuunga mkono
mabadiliko.
Chama kinaendelea kufuatilia kwa
karibu suala hili na taarifa zaidi zitatolewa kwa umma katika hatua za baadaye
kadiri iwezekanavyo.
Kurugenzi ya Habari na Uenezi
inatumia fursa hii kuwakumbusha watanzania wanaoishi nchini Marekani kuhudhuria
kwa wingi katika Mkutano wa CHADEMA utakaofanyika Maryland tarehe 27 Mei 2012
na kuwasiliana na Leticia Nyerere kupitia leticianyerere@rocketmail.com
kwa maelezo zaidi.
Imetolewa
tarehe 23 Mei 2012 na:
John
Mnyika (Mb)
Mkurugenzi
wa Habari na Uenezi
No comments:
Post a Comment