ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, May 24, 2012

TANZANIA YADHAMIRIA KUWEKA MAZINGIRA YA UPATIKANAJI WA MSAADA WA KISHERIA

:Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angela Kairuki akisoma hotuba wakati akifungua rasmi warsha ya  Mpango wa Msaada wa Kisheria Barani Afrika iliyoandaliwa na UNDP  na kuhudhuriwa na wadau wa masuala ya sheria kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika wakiwemo wenyeji Tanzania.
Katia ufunguzi huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam Mh. Kairuki amesema Serikali ya Tanzania imefanya jitihada mbalimbali za kuboresha huduma za misaada ya Kisheria haswa kwa watu ambao ni vigumu kuupata msaada huo, ambao wengi wao wanaishi katika maeneo ya vijijini.
Kauli mbiu ya Warsha hiyo ni " Taking Forward Legal Aid Programming in Africa: Experiences and Lessons in Policy and Programming".

Juu na chini ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Dk. Alberic Kacou akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya  Mpango wa Msaada wa Kisheria Barani Afrika iliyoandaliwa na UNDP.
Dk. Kacou amesema warsha hii ya Msaada wa Kisheria ni hatua nyingine katika kuelekea kuondoa vikwazo katika uwezeshaji wa Kisheria na kupatikana kwa haki kitu ambacho kimeathiri kwa kiwango kikubwa bara hili katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na maisha ya watu, mali, Uraia, huduma za kijamii na kukosekana kwa fursa za maendeleo. Kulia ni Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angela Kairuki na kushoto ni mmoja wa maafisa wa makao makuu ya UNDP New York Shelley Inglis.
Picha juu na chiniBaadhi ya wadau wa masuala ya sheria kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika wakiwemo wenyeji Tanzania wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Mh. Angela Kairuki.
Picha kwa hisani ya MO Blog

No comments: