Rais wa Mali, Dioncounda Traore.
WAANDAMANAJI wamemjeruhi na kumchania nguo Rais wa Mali, Dioncounda Traore.
Kutokana na kipigo hicho kiongozi huyo alikimbizwa hospitali ambako ilidaiwa kuwa alipoteza fahamu na kuzinduka baada ya muda.
Jeshi la nchi hiyo limethibitisha kuwa limewapiga risasi na kuwaua watu watatu miongoni mwa waandamanaji hao, wanaounga mkono mapinduzi ya serikali Machi mwaka huu.
Msemaji wa Jeshi, Bakary Mariko aliliambia Shirika la Habari la Uingereza (Reuters) kuwa “walimpiga sana na kuchana nguo zake.” Msaidizi wa karibu wa Traore aliliambia Shirika la Utangaza la Uingereza (BBC) kuwa Rais huyo alitibiwa majeraha kichwani na kuruhusiwa kurudi nyumbani.

Waandamanaji hao walikuwa na hasira kutokana na mpango wa kumweka madarakani Rais Traore (70) kwa kipindi cha mwaka mmoja. Muda wake kubaki ofisini ilibidi umalizike Jumatatu.
Viongozi wa nchi za Jumuiya ya Uchumi Afrika Magharibi (ECOWAS) walifikia makubaliano na kiongozi wa mapinduzi, Kapteni Amadou Sanogo kuwa Rais Traore abaki madarakani ili atayarishe uchaguzi, na kumaliza mgogoro wa waasi wa kaskazini.
Makubaliano mengine ni kuwa Kapteni Amadou Sanogo atambulike kama rais mstaafu, akipata mshahara wake na jumba la kuishi. Hata hivyo, katika kipindi cha maandamano, Kapteni Sanogo hajatoa kauli yoyote ya kuwataka waandamanaji wanaomuunga mkono watoke barabarani. Mapinduzi hayo pamoja na kuibuka kwa waasi wa eneo la kaskazini ya Mali, yamesababisha maelfu ya watu kuyahama makazi yao.
Mashirika yanayotoa misaada yanasema kuwa wanasikitishwa na ugumu wa utoaji huduma katika nchi ya Mali ambayo inakabiliwa pia na ukame. Mwandishi wa habari wa Bamako, Martin Vogi alisema kuwa askari waliwaruhusu maelfu ya waandamanaji kuingia katika Ofisi ya Traore ambayo iko jirani na Ikulu ya Rais. Vogi alisema kuwa watu waliwaunga mkono viongozi wa mapinduzi na kukasirishwa na wawakilishi wa tabaka la waliopinduliwa kuendelea kukaa madarakani kwa mwaka mmoja.
Walitaka mkutano mkuu uitishwe ili viongozi wa vyama ya siasa na mashirika yasiyo ya kiserikali kukaa pamoja kupendekeza kiongozi wa muda wa nchi hiyo. Wakati wa maandamano watu walibeba mfano wa jeneza la Traore wakilaumu ECOWAS na Dioncounda. Wasuluhishi wa nchi za ECOWAS waliondoka Bamako wakisema kuwa wamemaliza kazi.
Hata hivyo Msuluhishi Mkuu wa Bamako ambaye ni Waziri wa Nchi a Nje wa Burkina Fasso, Djibrill Basole alisema kuwa kiongozi wa mapinduzi atashauriana na Rais Traore na Waziri Mkuu wa Mali hadi hapo uchaguzi utakapokamilika mwakani. Wiki iliyopita, ECOWAS ilitishia kuwawekea vizuizi viongozi wa mapinduzi endapo wangeingilia siasa za nchi hiyo.
Kapteni Sanogo alianza kuitawala Mali tangu Machi mwaka huu na baada ya wiki tatu aliikabidhi kwa Traore, Spika wa zamani wa Bunge la Mali.
Ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa nchini Mali umesema kuwa kitendo hicho kimezidisha mashaka juu ya usalama wa nchi hiyo.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment