Maafisa watendaji wawili wa kijiji na kata na mwenyekiti wa kijiji wanashikiliwa na polisi wilayani Bunda kwa kudharau agizo la mkuu mpya wa wilaya ya Bunda la kushindwa kualika watu kuhudhuria mkutano wake wa hadhara wa kujitambulisha.
Wanaoshikiliwa katika kituo kidogo cha Kibara, ni Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Namuhura, Boniface Manyonyi (45), Kaimu Afisa Mtendaji wa Kijiji Namuhuru, Joseph Mfungo (60) na Mwenyekiti wa kijiji hicho, Mwinamila Kalyaya (46).
Viongozi hao wamekamatwa jana kufuatia agizo la mkuu huyo mpya wa wilaya ya Bunda, Joshua Mirumbe, baada ya kufika katika eneo la mkutano na kukuta wananchi wasiozidi 15, huku kukiwa hakuna hata mwenyekiti mmoja wa kitongoji.
Alisema kuwa kitendo cha kutokuwepo kwa wenyeviti wa vitongojia katika mkutano huo ni dalili tosha kwamba, viongozi hao hawakualika wananchi, licha ya kuagizwa kufanya hivyo.
Kufuatia hali hiyo mkuu huyo wa wilaya ya Bunda, alisema kuwa huo ni uzembe mkubwa kwa viongozi wa hao kushindwa kualika wananchi na ndipo akaamuru polisi wawakamate viongozi hao na kuwasweka ndani.
Alisema kuwa pamoja na mkutano huo ambao ni kwa ajili ya kujitambulisha kwa wananchi kutokana na kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, hivi karibuni kuwa mkuu mpya wa wilaya hiyo, lakini pia anatumia fursa hiyo kuhamasisha shughuli za maendeleo, ikiwa ni pamoja na kutaka kila mtu kwa nafasi yake atimize wajibu wake.
Katika hatua nyingine pia mkuu huyo wa Wilaya ya Bunda, pia jana hakufanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kasahunga, kutokana na idadi ya watu kuwa ndogo na diwani wa kata hiyo kuchelewa kufika katika eneo la mkutano.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment