ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, June 23, 2012

Majembe mapya Simba Mwanza



Klabu ya soka ya Simba, leo inawajaribu kwa mara ya kwanza wachezaji wake wote wapya waliosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu ya Bara katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Toto African, kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Kikosi cha Simba kipo mkoani humo kwa ajili ya ziara maalum ya kutembeza kombe la ubingwa kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Afisa Habari wa klabu hiyo, Ezekiel Kamwaga, alisema kuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo Richard Amatre amesema ziara hiyo imekuja wakati muafaka kwa ajili ya kuwangalia wachezaji wapya waliosajiliwa kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu.



"Kwa muda sasa wachezaji wapya walikuwa wakifanya mazoezi tu, sasa ni wakati muafaka wa kuwaangalia katika mechi," alisema Kamwaga akimnukuu kocha msaidizi wa klabu hiyo, Amatre.

Alisema wachezaji wote wapya watapata nafasi ya kucheza leo dhidi ya Toto pamoja na mchezo mwingine wa kesho dhidi bya Express ya Uganda.

Wachezaji hao wanaosubiliwa kuonyesha uwezo wao ni pamoja na Kigi Makasy, Mkongo Kanu Mbiyavanga, Paul Ngalema, Abdallah Juma, Ibrahim Rajabu 'Jeba' na Salum Kinje.
CHANZO: NIPASHE

No comments: