ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, June 23, 2012

Mfanye mwenzio apende unachokipenda

NAAM, kwa uwezo wa Muumba tumekutana tena kwenye kona yetu, binafsi sijambo, hofu kwako msomaji wa kona hii. Leo nizungumzie karaha katika mapenzi, nizungumzie starehe ya wanaume inavyogeuka karaha bila kujua.
Karaha zipi hizo?
Tunafahamu kila mtu ana starehe yake, wapo wanaopenda kupata moja moto moja baridi, wengine wapenzi wa kuvuta sigara, ugoro na vingine vingi.
Kila mtu ana haki ya kuchagua kitu anachokipenda, ikumbukwe kuwa matumizi ya vitu hivyo yakishindwa kuzingatia usafi huwa karaha ndani ya nyumba. Vitu hivi ni starehe za watu lakini upande mwingine huwa karaha kwa wengine wasiovitumia.
Karaha yake huja kipindi mnapokuwa pamoja, hasa wakati wa mapumziko ya kawaida pale midomo yenu inapokuwa karibu au kwenye maandalizi ya mapenzi, pale midomo yenu inapokutana. 

Asiyetumia kwake huwa karaha na kuogopa kumwambia mpenzi wake, pengine kutokana na ukali wake. Anayevuta sigara au kunywa pombe, anapokaa kwa muda mrefu mdomo hutoa harufu kali ambayo kwa yeyote asiyetumia vitu hivyo, huwa kero.
Unakuta mtu amerudi usiku akitoka kwenye starehe zake kama vile kwenye ulevi, anataka kula denda na mpenziwe bila kujali kama harufu ya mdomoni inamkera mwenza wake.
Lazima ifike hatua tubadilike tusitumie ubabe kwa wenzetu. Inawezekana umetoka kwenye ulevi au kuvuta sigara ukawa na hamu na mwenzio, bila kujua mdomo wako unatoa harufu kali unapanda kitandani na kumuomba denda. Kufanya hivyo ni karaha kwa mwenzako hasa akiwa hatumii vitu hivyo.
Kama unatumia ufanye nini?
Ukitoka kwenye ulevi, kuvuta sigara, kula kubeli au kuvuta ugoro, kabla ya kumsogelea mpenzi wako, lazima uusafishe mdomo kwa mswaki na dawa ili kuurudisha kwenye hali ya kawaida.
Hata kama umerudi usiku wa manane hakikisha una usafisha mdomo kwa mswaki na dawa. Hii itamfanya mpenzio asione kero kwa pombe au sigara zako na kuongeza upendo bila kuichukia starehe yako.
Lakini ukifanya kinyume cha hapo, elewa utamkosesha amani mkeo au mpenzi na kila atakapokuona umelewa au umeshikilia sigara, atakuwa akikosa raha.
Nina imani mvuta sigara na mtumiaji wa pombe utazingatia haya ili kuondoa karaha ndani ya nyumba yako na kuongeza upendo hata kufikia hatua ya mwenzako kukununulia sigara au chupa moja ili uchangamke.
Tofauti na hivyo, mpenzio au mkeo akiona sigara, lazima atazitupa au kuzitia maji.
Kwa hayo machache tukutane wiki ijayo.

www.globalpublishers.info

No comments: