Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume. |
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume, amesitisha mkutano wa hadhara uliyokuwa ufanyike jana kuzungumzia hali ya kisiasa ya Zanzibar kufuatia kuibuka kundi la watu wanaotaka Zanzibar kujitega na Muungano.
Kampeni za kutaka Zanzibar kujitenga katika mfumo wa muungano zimekuwa zikifanywa misikitini kwa zaidi ya miezi mitano na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya dini ya kislamu Zanzibar (Jumiki).
Kwa mujibu wa Uchunguzi wa NIPASHE, Mkutano huo, ulikuwa ufanyike katika viwanja vya Maisara Mkoa wa mjini Magharibi na kuhutubiwa na wanasiasa wakongwe Zanzibar akiwemo Rais mstaafu, wa Jamhuri ya Muungano, Ali Hassan Mwinyi.
Imedaiwa kwamba mkutano huo ulipangwa kufanyika baada ya kutokea shinikizo kubwa kutoka kwa viongozi CCM mikoa ya Zanzibar nawanachama ambao wanataka msimamo wa Chama juu ya kikundi cha Uamsho ambacho kinaendelea na kampeni za kutaka Zanzibar kujitenga katika wa Muungano.
Aidha, mkutano huo mbali na kuzungumzia hali ya kisiasa ya Zanzibar, pia ungezungumzia mchakato wa katiba mpya na mafanikio yaliyopatikana ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM tangu kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2010.
“Mkutano uliyokuwa ufanyike kuwajibu Uamsho wanaotaka Zanzibar kujitenga umesitishwa na Makamu Mwenyekiti Dk. Amani Karume,” alisema Kiongozi mmoja mwandamizi wa CCM Zanzibar.
Mkutano huo ambao ulipewa jina la “Mkutano wa kumtoa Paka katika Gunia” hulikuwa uhudhuriwe na wanachama wa CCM kutoka mikoa ya Zanzibar.
Mkutano huo uliandaliwa siku chache tangu Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja, Haji Juma Haji, kulalamika kwa nini waasisi wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, Zanzibar (SUK) Dk. Karume na Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad, kukaa kimya tangu Uamsho kuanza kampeni za kutaka Zanzibar kujitega katika Muungano na kusababisha hali ya kisiasa kuchafuka pamoja na makanisa na baa kuchomwa moto.
Katibu wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu (NEC) Idara ya Itikadi na Uenezi, Issa Haji Gavu, alithibitisha mkutano huo kuhairishwa kutokana na sababu mbali mbali, ikiwemo ikiwemo kujitokeza dharura kwa viongonzi waliotarajiwa kuhutubia mkutano huo.
Jumuiya ya Uamsho ambayo inaendelea na kampeni za kutaka kuitishwa kura ya maoni ili wananchi waulizwe wanautaka Muungano.

CHANZO: NIPASHE
5 comments:
wanawajibishwa hawa na serikali ya kanisa ha ha ha
lakini uzi ule ule haturudi nyuma, mpaka kieleweke
hatutaki muungano wa kikoloni wenye mfumo kiristo
karume si ananufaika na muungano so, nani wa kumsililiza tumeshachoka hata mkitupiga mabomu na kumwaga damu zetu lakin katu abadan inshallah muungano utakufa au utakuwa muungano wa MKATABA AMIN.
MOTO UMESHAWASHA NA KATU ABADAN HATUZIMIKA KWA MABOMU YENU YA MACHOZI NA VITISHO VYENU KAANI WAZI MKILIJUA HILI ILA UTAZIMWA NA SUB-HANA ALLAH WATAWALLAH AMIN
HAO WALIOUANZISHA HUO MUUNGANO WENYEWE WASHAKUFA SASA KWANINI MUUNGANO USIFE HATUUTAKI TENA HATUUTAKI HAKUNA KITAKACHIOBAKIA DUNIA ITAKWISHA SEUZE MUUNGANO TUMESHACHOKA NAO
Hayooo!!! Mawili magomvi!!! Chuki za kidini tu, wala hayana hoja za kuhusu muungano uwepo. au usiwepo,,na ma
badiliko yapi yafanywe kwa faida ya Wote?
Majitu mapenda vita, hamieni milimani kwa
wataliban mkapigane wee!! Mwishoni madrone ya USA. yawauwe, Tanzania si mahali penu nyie, tunapenda amani sisi.
Tanzania ndio nini? mnakataa jina lenu bure - nyie Tanganyka tu na muungano ulikuwa hivyo hadi mkamfanyia ujanja Karume na kumang'anya nchi kujiita Tanzania.
Hatutaki muungano wa kisiasa; tunataka wa kijamii. Mmezidiwa akili na magamba wanaiba Mabilioni na kuyapeleka Uswisi, hadi leo watoto wenu wanakaa chini bila madawati shuleni.
Amkeni magamba hawana haja ya Tanzania daini nchi yenu mufaidike, subirini mutakuja jikuta kama Nigeria; mna kila kitu lakini faida haionekani - Tanzanite inapatikana kwenu tu wapi fedha zinaenda? Dhahabu, Mbuga, Gesi na mafuta! Amkeni muwaondoe magamba mujenge nchi yenu musishughulike na Zanzibar tu, sisi habari ndio hiyo tunajikata kistaili - mupende musipende hata mleta jeshi lote la Muungano.Hatutaki Muungano wa dhulma.
Post a Comment