ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 26, 2012

SUPER D AITWA KUTOA UJUZI WA MASUMBWI IFAKALA,KILOMBERO


KOCHA wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila

'Super D' amepata mwaliko wa kwenda kufundisha  pamoja na kuwapati ujuzi aliokuwa nao katika mchezo wa masumbwi mwaliko huo alioupata kutoka mkoa wa Ifakala mjini Kilombero kutoka kwa klabu ya Kilombero Boxing Klabu  ambaye mwenyekiti wake ni Hiyari Bohari na katibu wa Klabu Hiyo ni Ramadhani Mindu wamempatia mwaliko wa siku mbili

Kocha huyo kwa ajili ya kuwanoa Makocha na kuwapatia ujuzi wa ziada mabondia chipukizi mwaliko huo unaomtaka kwenda kutoa ujuzi wa mchezo wa masumbwi kwa kushirikiana na kocha kutoka mkoa wa Morogoro Boma Kirangi mafunzo hayo yanayotakiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Agost yanaonekana kuwa na umuhimu kwa kuwa vijana wengi wamejitokeza kuwa na mwamko wa mchezo wa masumbwi nchini
Hata hivyo Super D 'alisema kuwa amepokea mwaliko kwa furaha na yupo tayali kutoa ujuzi wake alioupata wakati wa mafunzo ya kimataifa kwa vijana watakaojitokeza' Super D aliongeza kwa kusema mchezo wa maumbwi nchini unapendwa na wengi ila unakosa wafadhili kwa ajili ya kutoa sapoti mbali mbali Super D ametoa wito kwa makampuni mbalimbali  pamoja na wadau wa michezo kujitokeza kusaidia kwa namna moja au nyingine hususani mafunzo anayotaka kuyatoa akiwa mkoa wa Kilombero
Ambapo vijana wengi wanapenda kufahamu zaidi mchezo huo kwani kuna vijana zaidi walioamasika kucheza mchezo huo kwa kuwa na nia moja ya kuhakikisha mchezo wa masumbwi  unawafikisha mbali ya kuwa ni mchezo pia utawapatia ajira 
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Super D, alisema tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na mchanganyiko wa ‘clips’ za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.Super D, alisema mbali na michezo ya nyota hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali wengine DVD hizo zina michezo
ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibi Kinyogoli.”katika muendelezo wa kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli Foundition ” alisema. Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia  hii watu wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo. 

Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa
timu ya Ashanti na Amana kujifunza ‘live’ chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana
mbalimbali

RAJABU MHAMILA 'SUPER D' NA VISIBITISHO VYA KUWA KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI


CHETI CHA UTAMBULISHO WA KUFUZU MAFUNZO YA NGAZI YA KWANZA YA UKOCHA WA MASUMBWI KIRICHOTOLEWA NA SHIRIKISHO LA NGUMI ZA RIDHAA NCHINI TANZANIA BFT  KWA RAJABU MHAMILA 'SUPER D'
CHETI CHA UTAMBULISHO WA KUFUZU MAFUNZO YA NGAZI YA KWANZA YA UKOCHA WA MASUMBWI KIRICHOTOLEWA NA SHIRIKISHO LA NGUMI ZA RIDHAA NCHINI TANZANIA BFT  KWA RAJABU MHAMILA 'SUPER D'

CHETI CHA UTAMBULISHO WA KUFUZU MAFUNZO YA NGAZI YA JUU YA UKOCHA WA MASUMBWI  KIMATAIFA KIRICHOTOLEWA NA KAMATI YA OLIMPIC DUNIANI KWA KUSHIRIKIANA NA KAMATI YA OLIMPIC TANZANIA YA KUMTAMBUA SUPER D NI KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI

MOJA YA NEMBO INAYOTUMIWA NA SUPER D KUMTANGAZA KWA NJIA MBALIMBALI IKIWEMO FLANA ALIZOWAI KUTOA KWA MAKOCHA WENZIE WAKATI YUPO KATIKA MAFUNZO YA MCHEZO HUO KIMATAIFA

No comments: