ANGALIA LIVE NEWS

Friday, June 22, 2012

TANZANIA DMV KUCHEZA JUMAMOSI NA JUMAPILI


Timu ya Tanzania DMV leo Jumamosi June 23, 2012  itatupa kalata yake tena kwa kucheza na Romania katika mfululuzo wa ligi ya DMV  DIASPORA 2012 WORLD CUP mechi itakayochezewa kiwanja # 5 Greencastle, Maryland na mtanange huu unatarajiwa kuanza saa 9 alasili (3pm).

Timu yaTanzania DMV Kesho Jumapili June 24, 2012 itajitupa tena uwanjani kucheza na Timu ya Uingereza katika viwanja vya Germantown saa 12 jioni, mtanange huu utakua wa marudiano baada ya ule wa kwanza kuahirishwa kutokana na baadhi ya wachezaji wa Tanzania DMV kuchelewa kufika uwanjani kutokana na kupotea.

Mpaka sasa timu ya Tanzania DMV imeishacheza mechi 6, imeshinda 1 imedroo 2 na imefungwa mechi 3.

No comments: