Watu wawili akiwemo dereva wa pikipiki pamoja na abiria wake aliyetambuliwa kwa jina la Juma Ramadhani (25), mkazi wa Kibamba wamefariki kwenye ajali mbaya jijini Dar es Salaam, baada ya kugongana uso kwa uso na gari aina ya Toyota Hiace.
Dereva aliyefariki ambaye jina lake halikufahamika, ni mwenye pikipiki yenye namba T 299 BYZ baada kugongana na gari aina ya Toyota Hiace lenye namba T 292 AHM.
Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 2:00 asubuhi eneo la Magari Saba, Kibamba katika Wilaya ya Kinondoni.
Ajali hiyo ilisababisha wananchi kuziba barabara kwa kutumia magogo kwa muda wa nusu saa hadi polisi walipotokea.
Mashuhuda wa ajali hiyo walieleza kwamba pikipiki hiyo iligongwa na lori la mchanga na kusababisha igongane ana kwa ana na Hiace hiyo.
Hata hivyo, walisema kukosekana kwa matuta kumesababisha eneo hilo kuwa la hatari na hivyo kupoteza ndugu zao kwa ajali za mara kwa mara.
Kwa upande wake, askari wa Usalama barabarani wa Wilaya ya Kipolisi, Kimara aliyejitambulisha kwa jina moja la Ntilicha, alikiri kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa polisi walichelewa kupata taarifa kutokana na wananchi kutokuwa na namba za kituo hicho.
Aidha, baada ya Polisi kufika eneo la tukio, walichukua mwili wa marehemu pamoja na abiria aliyekuwa mahtuti na kuipeleka Hospitali Teule ya Tumbi, Kibaha.
Muuguzi wa zamu, Joyse Mfyuji, alikiri kumpokea Juma akiwa mahtuti lakini alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu.
Wananchi wa Magari Saba wameiomba serikali kuweka matuta kwenye eneo hilo kwa kuwa ajali nyingi zimekuwa zikitokea hapo.
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, Charles Kenyela, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba upelelezi unaendelea.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment